Matukio : Waziri , Mwigulu Nchemba afanya Mazungumzo na Balozi wa Uholanzi na Umoja wa Falme za Kiarabu - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


18 Nov 2016

Matukio : Waziri , Mwigulu Nchemba afanya Mazungumzo na Balozi wa Uholanzi na Umoja wa Falme za Kiarabu

 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (katikati) akimsikiliza Balozi wa Uholanzi nchini, Jaap Frederiks alipokuwa anamfafanulia jambo Waziri huyo ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo, walipokuwa wanajadiliana masuala mbalimbali ua ushirikiano kati ya Tanzania na Uholanzi. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Balozi Simba Yahya. Kulia ni Katibu wa Uchumi na Sera za Biashara wa Ubalozi huo nchini, Eugene Gies. 
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (kushoto)akimsindikiza Balozi wa Umoja wa Falme za Kiarabu, Abdulla Ibrahim Alsuwaidi mara baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliyofanyika katika ofisi ya Waziri Mwigulu, jijini Dar es Salaam leo.
 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (kulia) akimkaribisha ofisini kwake Balozi wa Uholanzi nchini, Jaap Frederiks kwa ajili ya kufanya mazungumzo naye kuhusu masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Uholanzi na Tanzania. Mazungumzo hayo yalifanyika katika ofisi ya Waziri huyo, jijini Dar es Salaam leo. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad