Waziri
wa Afya, Maeendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu
akiongea na wauguzi hawapo pichani wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi
katika jengo la kituo cha kuendeleza wauguzi na wakunga kitaaluma nchini
lililopo wilayani Kibaha leo Mkoa wa Pwani.
Waziri
wa Afya, Maeendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu
akikata utepe kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi katika jengo la kituo
cha kuendeleza wauguzi na wakunga kitaaluma nchini lililopo wilayani
Kibaha leo Mkoa wa Pwani.
Waziri
wa Afya, Maeendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu
katikati akiweka udongo kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi katika jengo
la kituo cha kuendeleza wauguzi na wakunga kitaaluma nchini lililopo
wilayani Kibaha leo Mkoa wa Pwani.
Waziri
wa Afya, Maeendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu
akiangalia michoro ya jengo litakavyokua pindi litakapomalizika wakati
wa uwekaji wa jiwe la msingi katika jengo la kituo cha kuendeleza
wauguzi na wakunga kitaaluma nchini lililopo wilayani Kibaha leo Mkoa wa
Pwani.
Mkuu
wa Wilaya ya Kibaha Bi. Assumpta Mshana aliyesimama akiongea na wauguzi
hawapo pichani wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi katika jengo la kituo
cha kuendeleza wauguzi na wakunga kitaaluma nchini lililopo wilayani
Kibaha leo Mkoa wa Pwani.
Msajili
Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania Bi. Lena Mfalila akiongea na
wauguzi hawapo pichani wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi katika jengo
la kituo cha kuendeleza wauguzi na wakunga kitaaluma nchini lililopo
wilayani Kibaha leo Mkoa wa Pwani.
Waziri
wa Afya, Maeendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wa
tatu kushoto akipata maelekezo kutoka kwa Msimamizi Elekezi wa mradi huo
Bw. Sauli Nkini Wa kwanza kulia kutoka Chuo Kikuu Ardhi wakati wa
uwekaji wa jiwe la msingi katika jengo la kituo cha kuendeleza wauguzi
na wakunga kitaaluma nchini lililopo wilayani Kibaha leo Mkoa wa Pwani,
wa pili kulia ni Msajili Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania Bi. Lena
Mfalila.
Wenyeviti
wa Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania wakimsikiliza kwa makini Waziri
wa Afya, Maeendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu hayupo
pichani wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi katika jengo la kituo cha
kuendeleza wauguzi na wakunga kitaaluma nchini lililopo wilayani Kibaha
leo Mkoa wa Pwani.
Wauguzi
mbalimbali wakimsikiliza kwa makini Waziri wa Afya, Maeendeleo ya
Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu hayupo pichani wakati wa
uwekaji wa jiwe la msingi katika jengo la kituo cha kuendeleza wauguzi
na wakunga kitaaluma nchini lililopo wilayani Kibaha leo Mkoa wa Pwani.
Habari/Picha Na Ally Daud.
Baraza
la Wauguzi na Wajunga nchini wametakiwa kutowaonea aibu wale wote
wanaoanzisha vyuo vya afya kama mradi wa kujiingizia fedha bila ya kuwa
na taaluma hiyo kwani kunapelekea kuhatarisha Maisha na afya za
watanzania.
Hayo
yamesemwa leo na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na
Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati akiweka jiwe la msingi katika jengo la
kituo cha kuendeleza wauguzi na wakunga kitaaluma nchini lililopo mjini
kibaha Pwani.
“Hatusemi
wasianzishe vyuo,bali vyuo vyote viwe vyenye hadhi ya kutoa wataalam
stahili ,visajiliwe na vikaguliwe mara kwa mara ili vizalishe wauguzi
wenye sifa na ujuzi stahili,uuguzi siyo ujasiliamali,hakikisheni
mnavifungia vyuo vyote feki ili tuweze kudhibiti utitiri huu” alisema
Waziri Ummy.
Aidha
Waziri Ummy alisema hivi sasa kumekuwepo na utitiri wa vyuo vingi vya
uuguzi ambavyo havijasajiliwa na havizalishi wauguzi ambao wanastahili
kuajiriwa kwenye sekta ya afya na hivyo kuhakikisha wanasimamia taaluma
hiyo na kuvifungia mara moja vyuo vilivyokosa sifa.
Waziri
Ummy alisema kuwa serikali inatambua na kuthamini mchango mkubwa
unaofanywa na wauguzi katika hospitali zote nchini hivyo maboresho
yatafanyika na kuhakikisha upatikanaji wa vitendea kazi kwa wauguzi.
“Asilimia
80 za kazi zote katika hospitali zetu nchini zinafanywa na wauguzi na
wakunga hivyo Serikali imesikia kilio chenu na tutahakikisha tatizo hili
tunalitatua” alisema Ummy.
Hata
hivyo Waziri Ummy aliwataka wauguzi kutekeleza wajibu wao kwa
kuzingatia maadili na viapo vyao vya kitaaluma kwa maendeleo ya Afya
nchini.
Kwa
upande wa Msajili wa Baraza la Uuguzi na Ukunga nchini Bi. Lena Mfalila
alisema jengo hilo linajengwa kwa awamu mbili ambapo awamu ya kwanza
limegharimu pesa ya kitanzania shilingi bilioni 2.2.
Aidha
Bi. Mfalila alisema kuwa ujenzi wa kituo hicho ulianza Desemba 2015 kwa
awamu ya kwanza na kiinatarajiwa kukamililika na kuanza matumizi yake
Januari2017.
No comments:
Post a Comment