Rais
wa Korea Kusini, Park Geun-hye amemtunuku nishani ya heshima aliyekuwa
Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Bw.Henry Clemens kwa kutambua juhudi zake
katika kuleta maendeleo katika vijiji vya Mfuru Mwambao na Njianne
kupitia mfumo Saemaul Undong (SMU) yaani kijiji kipya cha maendeleo.
SMU
ni mfumo uliotumika Korea katika kujiletea maendeleo mpaka sasa kufika
katika orodha ya nchi tajiri duniani. Mfumo huo unasisitiza swala la
wananchi wenyewe kufanya kazi kwa kujitolea kwa ajili ya maendenelo yao
wenyewe.Bw.
Clemens ambaye ni mwenyekiti wa SMU Tanzania alisema wazo hilo
alilipokea mwaka 2009 akiwa Mkuu wa wilaya ya Mkuranga na kulifanyia
kazi katika vijiji viwili na kuleta matokeo mazuri.
“kumekuwa
na maendeleo makubwa mara baada ya kutoa mafunzo kwa wanakijiji juu ya
thamani ya ardhi na umuhimu wa kufanya kazi kwa ushirikiano,” alisema
Bw. Clemens.Alisema
uzalishaji wa mazao kama mhogo, papai na nazi umeongezeka kwa asilimia
kubwa kutokana na ushirikiano wa wanavijiji wa Mfuru Mwambao na Njia
nne.
“Kujitolea
kwa wanakijiji katika kujiletea maendeleo kupitia dhana ya Saemaul
Undong ndio imetupatia heshima kubwa ya kutunukiwa nishani na Rais wa
Korea Kusini,” alisema Bw. Clemens.Akielezea
matumaini yake alisema ni muhimu dhana hiyo ya Saemaul Undong ikaenea
nchi nzima kwani inakwenda sawa na azma ya serikali ya kuondoa umasikini
kwa kufanya kazi kwa bidii.
Wakati
huo huo, Balozi wa Korea Kusini hapa nchini, Bw. Song Geum-Young
mwishoni mwa wiki ametembelea kijiji cha Njia nne na kujionea maendeleo
yaliyofikiwa na wananchi kwa kutekeleza dhana ya Saemaul Undong yaani
kijiji kipya cha maendeleo.“Nimejionea
maendeleo na changamoto hasa za miundombinu ya barabara na daraja
ambavyo ni muhimu katika kurahisisha usafirishaji wa watu na bidhaa
mbalimbali zinazozalishwa huku” alisema balozi huyo.
Alisema
Serikali ya Korea Kusini imejipanga katika kujenga miundombinu nchini
ili kurahisisha usafirishaji wa watu na bidhaa kutoka sehemu moja kwenda
nyingine katika kupata masoko ya bidhaa zao.Alisema
amefarijika sana na maendeleo waliyoyafikia wanakijiji hao na kuwaomba
waendelee kufanya kazi kwa bidii kwani mafanikio huja kwa kujitolea.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Msaidizi, Sekta za Uchumi na Uzalishaji toka
TAMISEMI, Dkt. Lucy Ssendi alisema atafikisha changamoto zinazowakabili
wananchi wa Njia Nne hasa ya kukamilishiwa daraja linalounganisha kijiji
hicho na Nyamihimbo.“Juhudi kubwa zimefanywa hadi sasa, nitafikisha taarifa hizo kwa mamlaka husika ili kufanikisha umaliziaji wa daraja,” alisema.
Mmoja
wa wanakijiji wa Njia nne Bi. Zuwena Kasinde aliishukuru serikali ya
Korea kwa kuchagua wilaya yao kuwa sehemu ya mfano wa mfumo wa SMU na
kusema kuwa watakuwa mfano kwa Tanzania katika maendeleo kupitia dhana
hiyo.
Mwenyekiti
wa Saemaul Undong Tanzania(SMU), Bw.Henry Clemens akikambidhi zawadi
kwa niaba ya wanakijiji wa Njianne, wilayani Mkuranga Balozi wa Korea
Kusini Nchini Bw.Song Geum-young alipotembelea katika kijiji hicho
kujionea maendeleo waliofikia kwa kupitia dhana ya Saemaul Undong yaani
kijiji kipya cha maendeleo ambayo ndio dhana iliyowafanya wao kupiga
hatua kiuchumi mpaka kufikia katika prodha ya nchi tajiri Duniani.
Katikati ni mwasisi wa SMU Mchungaji Joshua Lee
Mwenyekiti
wa Saemaul Undong Tanzania,(Mkuu wa Wilaya Mstaafu wa Mkuranga)
Bw.Henry Clemens akiwaonyesha waandishi wa habari (hawapo pichani)
medani ya heshima na cheti alichokabidhiwa na Rais wa Korea kusini Park
Geun-hye kwa kutambua mchango wake wa kuviendeleza vijiji vya Mfuru
mwambao na Njia nne vilivyopo Wilaya ya Mkuranga kupitia mfumo wa
saemaul undong( kijiji kipya cha maendeleo).
Balozi
wa Korea Kusini Nchini Tanzania Bw.Song Geum-young akipiga picha daraja
linalounganisha kijiji cha Njia nne na Nyamihimbo wakati waziara yake
katika kijiji hicho na kujionea maendeleo waliofikia kwa kupitia dhana
ya Saemaul Undong yaani kijiji kipya cha maendeleo ambayo ndio dhana
iliyowafanya wao kupiga hatua kiuchumi mpaka kufikia katika prodha ya
nchi tajiri Duniani. Kulia ni Mbunge mstaafu wa Mbinga Magharibi
Bw.Gaudence Kayombo. Kushoto ni mwasisi wa SMU Tanzania,Mchungaji Joshua
Lee. Wapili kushoto Mwenyekiti wa Saemaul Undong Tanzania Bw.Henry
Clemens
No comments:
Post a Comment