Michezo /Ngumi : Dullah Mbabe Ampiga kwa " Knockout" Mchina raundi ya kwanza - Wazalendo 25 Blog

Breaking

Glory to Story.


Post Top Ad


29 Oct 2016

Michezo /Ngumi : Dullah Mbabe Ampiga kwa " Knockout" Mchina raundi ya kwanzaBondia Abdallah  Pazi a.k.a Dullah Mbabe akimsukumia makonde mazito Bondia Chengbo Zheng kutoka nchini China na kupelekea mpambano huo kuisha ndani ya dakika mbili na sekunde kadhaa kwa 'KnockOut' ya kiufundi, katika Ukumbi wa Diamond Jubilee, Jijini Dar es salaam usiku huu.
Bondia Abdallah  Pazi a.k.a Dullah Mbabe akiendelea kumsukumia makonde mazito Bondia Chengbo Zheng yaliyompelekea kwenda chini na kuomba kutoendelea na mpambani huo.
Bondia Chengbo Zheng akimuomba msimamizi wake kumtoa 'Groves' baada ya kushindwa kuendelea na mchezo kufuatia makonde mazito na ya haraka haraka aliyoyapata kutoka kwa Bondia Abdallah  Pazi a.k.a Dullah Mbabe
Bondia Abdallah  Pazi a.k.a Dullah Mbabe (78.2KG) akitangazwa mshindi mara baada ya kumpiga kwa 'KnockOut' Bondia Chengbo Zheng (77.9KG) kutoka nchini China katika raundi kwanza kabisa ya mpambano wao usiokuwa wa Ubingwa uliomalizika usiku huu katika Ukumbi wa Diamond Jubilee, Jijini Dar es salaam.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi akimpongeza
Bondia Abdallah  Pazi a.k.a Dullah Mbabe kwa ushindi alioupata wa kumpiga Bondia Chengbo Zheng kutoka nchini China, na kufanya heshima ya mchezo huo kuendelea kubaki nchini.
Bondia Abdallah  Pazi a.k.a Dullah Mbabe akizungumza na vyombo vya habari.,
Katika mambano ya utangulizi, kulikuwa na pambano hili la raundi nane lililokuwa na mvuto wa aina yake lililowakutanisha mabondia Said Mbelwa (nyeupe) na Shaban Kaoneka. hili lilikuwa na pambano la rusha nirushe, ambapo Bondia Said Mbelwa alifanikiwa kushinda kwa 'KnockOut' ya kiufundi dakika ya saba ya mpambano huo.
Chukua hiyooooo...

Bondia Paul Kamata (nyeupe) akimsukumia makonde mithili ya mvua Bondia Buta Obed katika mpambano wao usio na ubingwa wa raundi nani, ulichezwa usiku wa leo katika Ukumbi wa Diamond Jubilee, Jijini Dar es salaam. Bondia Paul Kamata alishinda kwa 'KnockOut' ya kiufundi, katika raundi ya tano ya mchezo hio.


Post Top Ad