Mkurugenzi
Mkuu wa Mfuko wa Pensheni (PSPF) Adam Mayingu, akizungumza na wanachama
wa Chama Cha Walimu Wastaafu jiji la Tanga (Chajiwata) wakati wa
maadhimisho ya wiki ya Huduma kwa Mteja jana. kulia anaemwangalia ni
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigella.
Mkurugenzi
Mkuu wa Mfuko wa Pensheni (PSPF) Adam Mayingu, akipokea Hati na Katiba
ya Chama Cha Walimu Wastaafu jiji la Tanga (Chajiwata) kutoka kwa
aliekuwa Afisa Elimu shule ya Msingi jiji la Tanga, Damass Kifanga.
Wanachama
wa Chama Cha Walimu Wastaafu jiji la Tanga (Chawajita) , wakifuatilia
hotuba ya mkurugenzi mkuu wa Mfuko wa Pensheni (PSPF), Adam Mainga,
wakati wa maadhimisho ya wiki ya huduma kwa mteja kwa walimu wastaafu
uliofanyika Tanga jana.
Mkuu
wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigella, akifungua mkutano wa wanachama wa
Chama Cha Walimu Wastaafu jiji la Tanga, (Chawajita) wakati wa
maadhimisho ya wiki ya huduma kwa mteja wa Mfuko wa Pensheni (PSPF)
uliofanyika Tanga
Mwenyekiti
wa Chama Cha Walimu Wastaafu jiji la Tanga, (Chajiwata) Debora Daffa,
akizungumza katika mkutano wa Mfuko wa Pensheni (PSPF) wakati wa
maadhimisho ya wiki ya huduma kwa mteja mkutano uliofanyika Tanga jana.
Mwanachama
wa Chama Cha Walimu Wastaafu jiji la Tanga (Chajiwata) Roda Matoi,
akizungumza katika mkutano wa Mfuko wa Pensheni (PSPF) na walimu
wastaafu wakati wa maadhimisho ya wiki ya huduma kwa mteja na kufanyika
ukumbi wa mikutano jengo la Mkuu wa Mkoa wa Tanga jana
Viongozi
wa Chama Cha Walimu Wastaafu jiji la Tanga (Chajiwata) pamoja na STAFF
ya Mfuko wa Pensheni (PSPF) wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa
Mkoa wa Tanga, Martin Shigella mara baada ya mkutano na walimu wastaafu
wakati wa maadhimisho ya wiki ya huduma kwa mteja mkutano uliofanyika
jana ukumbi wa mikutano jengo la Mkuu wa Mkoa.
Na blog ya kijamii tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment