Mkurugenzi
Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Adam Mayingu, (kushoto), akimsikiliza
Mwanachama wa Mfuko huo, Margareth Mpunga, aliyefika kuhudumiwa wakati wa Wiki
ya PSPF kwenye kitengo cha huduma kwa wateja makao makuu ya Mfuko jijini Dar es
Salaam, Oktoba 4, 2016. Wakurugenzi na Mameneja
wakiongozwa na Mkurugenzi Mkuu, waliungana nawafanyakazi wa kitengo hicho kuwahudumia wateja ikiwa ni sehemu ya shamrashamra za wiki hiyo inayofikia kilele Oktoba 7
Meneja wa Kitengo cha Huduma kwa wateja cha PSPF, Laila Maghimbi, (kushoto), akimuhudumia mteja ofisini kwake Oktoba 4, 2016Judith Mtweve wa kitengo cha mawasiliano (call centre), akiwa kazini
Meneja wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja, akimsikiliza mteja
Mkurugenzi Mkuu, akimsikiliza kwa makini mteja
NA
K-VIS BLOG/Khalfan Said
WANACHAMA
wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, wamepongeza uongozi wa Mfuko huo, kwa huduma bora
na za haraka katika kuhudumia wateja.
Hayo
wameyasema Oktoba 4, 2016 wakati wa Wiki ya Huduma kwa Wateja, kwenye makao
makuu ya Mfuko huo jengo la Jubilee Towers jijini Dar es Salaam.
“Nimefurahishwa
na huduma zilizokuwa zikitolewa, kwani nilipofika nimepokelewa na kuhudumiwa
haraka, sikuchelewa, kilichonileta ni kuwasilisha risiti za benki za michango
yangu,” alisema Mwanachama wa PSPF kupitia mpango wa uchangiaji wa Hiari,(PSS),
Hamid Maxan Haidary.
Hata
hivyo mwanachama huyo alishauri, Mfuko ufanye juhudi kuelimisha umma hususan
wajasiariamali kama yeye wajiunge nao kwani anahakika wengi watajiunga.
“Wafanyakazi
wapelekwa huko kwenye kata, najua zipo juhudi kubwa za kufanya matangazo kwenye
radio/tv, magazeti na mitandao ya kijamii, lakini sio vibaya wafike wenyewe
mitaani kutoa elimu zaidi.” Alishauri.
“Mimi
kama mtu mwenye kipato cha chini, nilikuwa Napata shida sana inapokuja swala la
kuugua au kuuguliwa na watoto au mke wangu, lakini hivi sasa hilo sio tatizo
tena kwangu, kwani kupitia bima ya afya ambayo nimepata baada ya kujiunga na
PSPF, ninatibiwa bila wasiwasi.” Alifafanua Haidary.
Mwanachama
mwingine wa Mfuko huo ambaye ni mstaafu, Peter Protus Mbele (64), alielezea
kufurahishwa kwake na faida anayopata kutoka PSPF yeye kama mstaafu, ambapo
licha ya kuchukua pensehni ya kila mwezi, ameweza pia kukopa fedha benki na
hivyo kuboresha shughuli zake.
“Kwa
ujumla nafurahia huduma za PSPF, nimeweza kupata mkopo benki, panatokea mara
chache kuchelewa kwa palipo ya mwezi ya pensheni, lakini mimi nachukulia kama
ni changamoto ya kawaida, kwani hata nyumbani mama anaweza kuchelewa
kutayarisha chakula, pengine kwa sababu kuni ni mbichi au mkaa hauko vizuri
lakini hatimaye chakula kinawiza na mnakula,” alisema.
Naye
Devotha R. Kayumbe, aliusifu uongozi wa PSPF kwa kuwajali wateja. “Nimejisikia
raha kuhudumiwa na Mkurugenzi Mkuu, hii inaonyesha jinsi watumishi wa umma
wanavyowajibika na kwenda sambamba na kasi dhana ya Hapa Kazi Tu.”. Alisema
Kayumbe.
Naye
Naomi Albert Duma, ambaye alifika kwa nia ya kujiunga na Mfuko kupitia Uchangiaji
wa Hiari, (PSS), alisema, ameridhishwa na huduma aliyopata kwani amehudumiwa
kwa haraka na hakutegemea kama angechukua muda mfupi kumaliza kile kilichomleta.
“Nimefika
kujiunga na PSS, tayari nimehudumiwa na sasa naondoka.”Alisema .
Akizungumzia
Wiki ya Huduma kwa wateja, Meneja wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja cha PSPF,
Laila Maghimbi, alisema, kila mwaka wiki ya mwanzo ya Oktoba Dunia huadhimisha
Wiki ya Huduma kwa Wateja. “Kuanzia Oktoba 3 hadi 7 tutakuwa tukiadhimisha wiki
hii, kwa viongozi mbalimbali wa Mfuko, kupita maeneo mbalimbali ya nchi
kuungana na wafanyakazi wa huko na kuhudumia wateja.” Alifafanua.
Meneja
huyo alisema, katika wiki hii wateja pia watapata fursa ya kutoa maoni yao ili
Mfuko uweze kuyafanyia kazi kwa nia ya kuboresha huduma, alisema.
Baadhi
ya wakurugenzi na mameneja wakiongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Adam
Mayingu, waliungana na wafanyakazi wa kitengo cha huduma kwa wateja, ili kutoa
huduma kwa wanachama waliofika kupatiwa huduma.
Mkurugenzi
mkuu alipata fursa ya kutoa huduma kwa muda wa dakika 35 na baadaye kutoa barua
za pongezi kwa wafanyakazi bora watatu wa kitengo hicho.
Wafanyakazi
hao ni pamoja na Afisa Huduma kwa wateja, January Buretta, Afisa Mwandamizi wa
Uendeshaji, Hilda Mwema na Afisa Mkuu wa Matekelezo, Matilda Nyallu.
Alitolea
mfano hapo makao makuu ambapo Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko, Adam Mayingu, naye
aliungana na wafanyakazi wa kitengo chake kuhudumia wateja.
“Sambamba
na kutoa huduma, lakini pia Wiki hii tutaitumia kuwatunukia wafanyakazi wetu
bora katika kitengo hiki.” Aliongeza
Mkurugenzi Mkuu, akimsikiliza Mteja, Devotha Kayumbe
Meneja wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja, Laila Maghimbi, (kushoto), akimuhudumia mteja
Mkurugenzi Mkuu, akimkabidhi barua ya pongezi, Mmoja kati ya wafanyakazi watatu bora wa ,kitengo hicho, January Buretta, ambaye ni Afisa mwandamizi Huduma kwa wateja wa PSPF
Mkurugenzi Mkuu akimkabidhi barua ya pongezi, Afisa Mkuu wa Matekelezo, Matilda Nyallu
Mkurugenzi Mkuu akimkabidhi barua ya pongezi, Afisa Mwandamizi wa Uendeshaji, Hadija Mwema |
Mkurugenzi wa Uendeshaji, wa PSPF, Neema Muro, (kulia), akifuatilia jinsi Afisa Uendeshaji Mkuu wa Mfuko huo, Zeinab Dau, (wapili kulia), wakati akimuhudumia mteja
Meneja Matekelezo wa PSPF, Francis Mselemu, (kushoto), akimuhudumia mteja
Mkurugenzi wa ukaguzi wa ndani, Sosthenes Mushema, (kulia), akimsikiliza kwa makini mteja aliyefika kuhudumiwa Oktoba 4, 2016 |
Afisa mwandamizi msaidizi wa nyaraka, Gwamaka Ngomale, (kushoto), akimuhudumia mteja |
Wateja wakipatiwa huduma na wafanyakazi wa PSPF
Wafanyakazi wa PSPF, sehemu ya call centre wakitekeleza wajibu wao
Picha ya pamoja
Paulina Kagaruki, (kulia), Afisa uendeshaji, akimhudumia mteja
Isack Kimaro, (kushoto), akimuhudumia mteja
Afisa wa Uendeshaji wa PSPF, Elizabeth Shayo, akimhudumia mteja Oktoba 4, 2016
Hadji Jamadary (kulia), akimuhudumia mkuu wa wilaya wa zamani Lephy Gembe, aliyefika kupata huduma za PSPF Oktoba 4, 2016
Afisa Mkuu Huduma kwa Wateja wa PSPF, Queen Edward, (kulia), akimuhudumia mteja.
No comments:
Post a Comment