====== ======= ======== Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mh. Godwin Gondwe na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Bw. William Makufwe wamepiga marufuku ufugaji holela. Tamko hilo limetolewa baada ya uongozi wa kijiji cha Chogo Kata ya Kabuku Ndani kuomba Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi Mtendaji kuwasaidia kuondoa wafugaji waliovamia katika kijiji chao na kuharibu mazao ya kilimo ya wananchi wa kijiji hicho.
Akizungumza
na wananchi hao Mkuu wa wilaya aliwaeleza wananchi kuwa kila sehemu
kuna taratibu na sheria zake namna ya kuishi. “ni marufuku kuchunga
mifugo kwenye maeneo ya hifadhi ya misitu ya Serikali au ya Kijiji kwa
maana ni kosa akipatikana mtu wa namna hiyo kamateni peleka polisi na
mimi nifahamu”alisema, na pia ni marufuku kuchukua mifugo kwenda
kuchunga kwenye shamba la mwenzako kuwepo na mazao au hakuna ni kosa
kamateni mtu wa namna hiyo peleka polisi, hata kama mwenye shamba
amekwisha vuna isipokuwa kwa idhini ya mwenye shamba pekeyake.
Mkurugenzi
mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni aliwaeleza
wananchi kwamba ulinzi wa mali za Chogo ni wanachogo wenyewe, na
mgogoro wa wakulima na wafugaji ni wetu sote, Aliwaeleza kwamba
walishindwa kuchukua tahadhari mapema pindi wafugaji hao walipoingia
miezi mine iliyopita kwa sababu eneo lao lina mpango bora wa matumizi ya
ardhi.
Aidha
aliwaeleza wananchi kuwa, amewataka Watendaji wa Kata na Vijiji kuleta
orodha ya mifugo iliyopo kwenye maeneo yao na waeleze uwezo wa ardhi
iliyopo kuweza kuhimili idadi ya mifugo iliyopo kwa mujibu wa mpango wa
ardhi uliowekwa katika maeneo yao ili kugungua kama kunamifugo imezidi
au haijazidi, “Tarehe 29/10/2016 nitapata orodha ya Halmashauri nzima
kwa kata 21 na Vijiji 91” alisema.
Mfugaji
wa mwanzo ambae atakuwepo katika kijiji husika kwa kumkaribisha ama la
kama idadi ya mifugo aliyokuwa nayo inakidhi viwango atabaki, lakini kwa
mfugaji atakaye zidisha kiwango cha mifugo basi ataondolewa ili
aende kutafuta mahali kwingine na marufuku kukaribisha mfugaji mwingine
alisema Mkurugenzi.
Mwenyekiti
wa kijiji cha Chogo aliwaeleza viongozi kuwa wafugaji hao waliingia
kwenye maeneo yao bila kufuata utaratibu, wameleta uharibifu wa mazao
napindi wanapohitajika kwenye vikao ili wapewe utaratibu wanakaidi
kufika. Alieleza kuwa eneo ambalo limetengwa kaajili ya mifugo lipo eneo
la Chang’ombe na kwa mujibu wa idadi ya mifugo iliyopo tayari
imejitosheleza. Mifugo iliyovamia ni zaidi ya 4000 na kwamba ardhi ya
kijiji haiwezi kutunza idadi kubwa ya mifugo.
Bw.
Said Mmbelwa mwanakijiji wa Chogo kitongoji cha Kibamba aliwaeleza
wananchi wenzake kuwa walifanya makosa kuwakaribisha wafugaji hao bila
kufuata utaratibu na kwamba kama wananchi weneyewe wasipobadilika basi
migogoro ya wakulima na wafugaji haitakwisha.
Aidha
Diwani wa kabuki ndani Mh. Abdallah Pendeza aliwashukuru Mkuu wa
Wilaya na Mkurugenzi Mtendaji na Kuwataka wananchi kutekeleza yale
ambayo viongozi wamewaelekeza kwa kushirikiana, kwamba kila mmoja
atimize wajibu wake kulingana na sheria, taratibu na kanuni.
Mkuu
wa Wilaya aliwataka viongozi wa vijiji kuhuisha kamati za ulinzi na
usalama na kuhakikisha wanaripoti kwenye vyombo vya sheria pindi
wanapoona kunamtu ameingia kwenye maeneo yao haeleweki ili kulinda
amani.
Imetolewa na
Alda Sadango
Afisa Habari
Halmashauri ya Wilaya Handeni
No comments:
Post a Comment