Jamii ya Wamasai kutoka Wilaya ya Simanjiro wakiwa katika sherehe za
kuhama rika ambapo wananchi 600 walihama rika na kuamia rika la wazee
maarufu kama Korianga .Picha na Ferdinand Shayo
Na Ferdinand Shayo wa Wazalendo 25 Blog ,Simanjiro.
Viongozi wa
Mila wa jamii ya Wamasai wametakiwa kusuluhisha na kutatua migogoro ya ardhi,maeneo ya malisho pamoja na wizi wa
mifugo ili kuepusha uvunjifu wa amani na kuzorota kwa maendeleo
kunakosababishwa na migogoro hiyo.
Hayo
yameelezwa na Wazee wa Mila Peter Toima na Lemamiye Shininii wakati wa sherehe
za kuhama rika ambao Maelfu wa
vijana kutoka Wilaya ya Simanjiro
wanahamia rika la wazee na kukabidhiwa wajibu wa kuwa wasuluhishi katika jamii.
Wazee hao
Walisema kuwa jukumu la kutatua migogoro linapaswa kufanywa na Wazee hao wapya na kuepuka kuitwisha serikali mzigo
mkubwa wa migogoro ambayo wangeweza kuitatua .
Kwa upande
wao Vijana waliohama rika na kuingia rika la wazee Oreka Mlolo na walisema kuwa
kazi kubwa iliyoko mbele yao ni kuhakikisha kuwa jamii inaishi kwa amani
,kudumisha umoja na ushirikiano ambazo ni tunu muhimu kwa jamii ya Wamasai.
Mmoja wa
Kinamama ambao Waume zao wameama rika Loema Thadey alisema kuwa mila hiyo
hutumika kupima uaminifu wa Wanandoa
iwapo Mwanamke anachepuka basi anaweza kupoteza maisha.
Jamii ya
Wamasai ni jamii yenye tamaduni yenye nguvu iliyodumu kwa muda mrefu na
kuenziwa licha ya changamoto ya utandawazi uliomeza tamaduni nyingi za Kiafrika
na kuleta utamaduni wa nchi za Magharibi.
No comments:
Post a Comment