Maatukio : Upelelezi Kinondoni kuisha ndani ya Siku Sitini - Wazalendo 25 Blog

Breaking

Glory to Story.


Post Top Ad


4 Oct 2016

Maatukio : Upelelezi Kinondoni kuisha ndani ya Siku Sitini


Mkuu wa mkoa wa Morogoro Mhe. Dkt Kebwe Stephen Kebwe akipokewa na mkuu wa kitengo cha Kuboresha usalama wa jamii ( DCP) Godluck Mongi alipokwenda kufungua mafunzo ya upelelezi kwa askari wa polisi 100. ( katika ni mkuu wa mafunzo wa Jeshi la Polisi DCP Ally Lugendo. Mafunzo hayo yanafanyika katika chuo cha polisi kidatu yamefadhiliwa na Tasisi ya Hanns Sidel. Picha na Tamimu adam- Jeshi la Polisi.
Mkuu wa mkoa wa Morogoro Mhe. Dkt Kebwe Stephen Kebwe( katikati) akiimba wimbo wa maadili wa ofisa wa Polisi wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa mafunzo ya upelelezi yanayofanyika katika chuo cha polisi kidatu. Mafunzo hayo kwa askari 100 yamefadhiliwa na Taasisi na Hanns Sidel.
Mkuu wa mkoa wa Morogoro Mhe. Dkt Kebwe Stephen Kebwe) akiingia katika ofisi ya mkuu wa chuo cha Polisi Kidatu kuzindua mafunzo ya upelelezi kwa askari polisi 100. Mafunzo hayo ya upelezi yamefadhiliwa na Taasisi na Hanns Sidel.
Mkuu wa mkoa wa Morogoro Mhe. Dkt Kebwe Stephen Kebwe) akisalimiana na wakufunzi wa chuo cha polisi kidatu alipokwenda kuzindua mafunzo ya upelelezi.Mafunzo hayo ya upelezi yamefadhiliwa na Taasisi na Hanns Sidel. (picha na Tamimu Adam – Jeshi la Polisi)

Na. Tamimu Adam - Jeshi la Polisi

Mkuu wa mkoa wa Morogoro mhe. Dkt Kebwe Stevin kabwe amesema Jeshi la polisi Tanzania ni kioo kwa majeshi ya polisi yalipo Afrika mashariki na hata afrika kwa ujumla kutokana na umahili wake wa kutoa mafunzo mbalimbali ya uaskari kwa baadhi ya nchi zilizopo afrika mashariki .

Dkt Kebwe aliyasema hayo wakati wa uzinduzi wa mafunzo ya miezi miwili ya upelelezi katika chuo cha Polisi kidatu yaliyofadhiliwa na Taasisi ya Hanns Sidel kwa askari polisi 100 waliotoka katika mkoa wa kipolisi kinondoni ambalo wamechaguliwa kwa ajili ya kutekeleza kwa weledi mpango wa kuborewsha usalama wa jamii unaoendelea kutekelezwa katika mkoa huo wa kipolisi.

“Huwezi kwenda kujifunza katika nchi ambayo haifanyi vizuri, na ndioo maana nchi za jirani huja Tanzania kwa ajili ya kujifunza namna Jeshi la Polisi Tanzania linavyo weza kuimarisha usalama wa raia na mali zao” alisema Dkt Kebwe.

Aliwataka askari hao wanafunzi wa upelelezi kujifunza kwa makini ili kuboresha umahiri walionao katika kufanikisha upelelezi ili kuweza kuleta mabadiliko ya kivitendo katika mkoa wa kinondoni kama eneo la mfano na hatimaye maboresho hayo yaweze kuenea na kutekelezwa katika mikoa yote nchini hivyo kuimarisha usalama wa raia na mali zao.

Kwa upande wake mkuu wa kitendo cha kusimamia mapango huo wa kuboresha usalama wa jamii kutoka makao makuu ya Polisi Naibu kamishina wa Polisi ( DCP)Godluck Mongi alisema mafunzo hayo ya upelelezi yataleta mafanikio makubwa katika mkoa huo wa kinondoni kwa kuharakisha upelelezi wa kesi na hakuna kesi itakayocheleweshwa chini ya siku sitini kwa maana hiyo ndani ya siku sitini upelelezi wa kesi inatakiwa iwe imeisha.

Aliongeza kuwa lengo la maboresho hayo ni kuhakikisha ifikapo mwaka 2019  askari wote upelelezi wawe wamepata mafunzo hayo ili waweze kuandana na kasi inayotakiwa katika mpango huo wa maboresho ya usalama wa jamii. 

Naye mwakilishi wa taasisi inayofadhili mafunzo hayo, Bw. Ombeni mhina lisema kwamba, ufadhili wa mafunzo ya upelelezi kwa askari polisi 100 kutoka mkoa wa kipolisi kinondoni ni sehemu ya mpango wa Taasisi ya Hanns Seidel kuunga mkono jitihata za jeshi la polisi katika kuimarisha ulinzi na usalama kwa raia na mali zao kupitia mpango wa kuboresha usalama wa jamii unaoendelea kutekelezwa katika mkoa wa kipolisi kinondoni.

Aliongeza kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi sitini ambazo jumla ya miradi 100 inaendelea kutekelezwa ikiwa na lengo la kukuza demokrasia, amani na maendeleo duniani kote.

Kwa upande wake mkuu wa chuo cha Polisi Kidatu kamishina Msaidizi wa Polisi ( ACP) Andrea Mwang’onda aliwataka wanafunzi wanapata mafunzo hayo ya upelelezi kuzingatia kile wanachofundishwa na kufuta maadili yote ya uaskari wakati wote watakapokuwa katika mafunzo hayo.

Post Top Ad