Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani Hamad Masauni (Mb), (Wa kwanza kulia) akipokea
maandamano katika maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani
yaliyofanyika mkoa wa Geita. Wa pili kushoto ni Naibu Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Edwin Ngonyani.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani Hamad Masauni (Mb) akisalimiana na mmoja wa
walemavu aliyejitokeza kushiriki katika maadhimisho ya Wiki ya Nenda
kwa Usalama Barabarani kitaifa, Mkoa wa Geita.
Mmoja
wa watumishi kutoka wizara ya ujenzi,uchukuzi na Mawasiliano akitoa
elimu kwa wanafuzi wa shule ya msingi kalangalala walipotembelea banda
la wizara hiyo wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama
kitaifa mkoani Geita.
Kikosi
cha Brass Band kutoka Serengeti Mkoani mara kikitumbuiza wakati wa
maadhimisho ya wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani ambayo kitaifa
yamefanyika mkoa wa Geita.
Waendesha pikipiki (boda boda) mkoa wa Geita wakiwa katika maandamano ya maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama kitaifa.
No comments:
Post a Comment