Mchungaji King James wa Kanisa la
Pentekoste Assemblies of God (P.A.G) kutoka Maeneo ya Kahororo Kyamaizi
Bukoba, King James ambaye pia ni mmoja wa wadau mmoja wa wadau wa
maendeleo Manispaa ya Bukoba Leo jumatano septemba 14, 2016 jioni
amewatembelea Waathiriwa wa Tetemeko na kuwafariji Wananchi. Ni baada ya
maafa kutokea katika janga la tetemeko la ardhi, lililotokea jummosi
iliyopita mkoani hapa Kagera, ambapo imeripotiwa idadi ya vifo
kuongezeka na kufikia watu 17, huku wengine 253 wakijeruhiwa na
kusababisha simanzi na masikitiko kwa familia nyingi. Katika tukio hilo,
pia nyumba 840 za makazi zimeanguka, nyumba 1,264 zimepata nyufa kubwa
na majengo 44 ya taasisi mbalimbali zikiwemo shule kuanguka.
King
James ametembele sehemu tofauti tofauti kama Kata ya Hamugembe, Kashai,
Rwamishenye na kutoa Misaada ya dharura kama Mahema, mchele, Sukari na
Pesa taslimu na kuwaombea pia. Mchungaji James pia kesho ataendelea
kutoa Misaada kwa Wahanga wa Tetemeko la Ardhi la nguvu ya 5.7 katika
vipimo vya Richter lilitokea eneo la Bukoba, kaskazini magharibi mwa
Tanzania ambalo limeathiri sehemu kubwa ya Wanakagera kuanzia kwenye
Makazi yao na wengine kukosa makazi na mpaka sasa kulala nje kutokana na
nyumba zao kubomolewa.
Takribani
shilingi bilioni 1.4 zimepatikana mpaka sasa katika harambee
iliyoongozwa na serikali ili kusaidia athari za tetemeko la ardhi hapa
mkoani Kagera. 
Hamugembe Omukishenye ni sehemu kubwa iliyoathiriwa na tetemeko la Ardhi
na Nyumba Nyingi kuanguka na nyingi kubomoka huku ikiwa imepoteza zaidi
ya Wakazi 6.
Furaha kwa Mama Saada mama Mlezi wa Watoto Yatima baada ya kutembelewa
na kupokea Misaada, Na hapa akiwashukuru wageni hao waliompatia msaada
huo wa Dharura katika kipindi hiki kigumu kinachowalaza nje baada ya
Nyumba yao kuangushwa na Tetemeko la Ardhi lililotokea Jumamosi septemba
10, 2016.
No comments:
Post a Comment