Mkurugenzi
Mkuu wa Airtel, Bwn Sunil Colaso akiongea na waandishi wa habari
wakati wa uzinduzi wa ushirikiano kati ya Airtel na PUMA utakaowawezesha
wateja kulipia bidhaa na huduma za PUMA kupitia Airtel Money TapTap.
Mkurugenzi
Mkuu wa Airtel, Bwn Sunil Colaso (kulia) na Meneja mkuu wa Puma Energy,
Philippe Corsaletti wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya
kusaini makubaliano rasmi ya ushirikiano mpya ambao unawawezesha
wateja kulipia bidhaa na huduma zote za Puma Energy kwa kutumia kadi ya
“Airtel Money Tap Tap” katika vituo vya mafuta vya PUMA nchini.
Mkurugenzi
Mkuu wa Airtel, Bw. Sunil Colaso (kulia) na Meneja Mkuu wa Puma Energy,
Philippe Corsaletti wakisaini mkataba wa makubaliano rasmi ya
ushirikiano mpya ambao unawawezesha wateja kulipia bidhaa na huduma
zote za Puma Energy kwa kutumia kadi ya “Airtel Money Tap Tap” kwenye
vituo vyao vya mafuta vya PUMA nchini. Wakishuhudia (kushoto) Meneja
Bidhaa wa Puma , Adam Sipe na Meneja Mauzo wa Airtel, Bi Bartleth Omari.
Mkurugenzi
Mkuu wa Airtel, Bw. Sunil Colaso (kulia) na Meneja mkuu wa Puma Energy,
Philippe Corsaletti wakibadilishana mikataba mara baada ya kusaini
makubaliano rasmi ya ushirikiano mpya ambao unawawezesha wateja
kulipia bidhaa na huduma zote za Puma Energy kwa kutumia kadi ya “Airtel
Money Tap Tap” katika vituo vya mafuta vya PUMA nchini kote.
Wakishuhudia (kushoto) Meneja Bidhaa wa Puma , Adam Sipe na Meneja Mauzo
wa Airtel, Bi Bartleth Omari
Meneja
kitengo cha Airtel Money, Asupya Naligingwa, akitoa maelezo jinsi ya
kuweka na kulipa mafuta kupitia kadi ya Airtel Tap Tap wakati wa
uzinduzi wa ushirika mpya kati ya Airtel na PUMA utakaowezesha wateja
kulipia bidhaa na huduma zote za PUMA energy kwa kadi maalumu
iliyounganishwa na huduma ya Airtel Money ya Tap Tap. Pichani ni mpiga
picha mkuu wa jambo leo, Richard Mwaikenda akiwekewa mafuta na muhudumu
wa kituo cha PUMA oyesterbay kupitia huduma ya Airtel Tap Tap wakati
wa uzinduzi huo
Meneja
kitengo cha Airtel Money , Asupya Naligingwa akiongea na Mkurugenzi
Mkuu wa Airtel, Bwn Sunil Colaso (kulia) na Meneja mkuu wa Puma Energy,
Philippe Corsaletti mara baada ya uzinduzi wa huduma ya Airtel Tap Tap
katika vituo vya puma.
Meneja
mkuu wa Puma Energy, Philippe Corsaletti akiongea na waandishi wa
habari wakati wa uzinduzi wa ushirikiano kati ya Airtel na PUMA
utakaowawezesha wateja kulipia bidhaa na huduma za PUMA kupitia Airtel
Money TapTap
Puma Energy kupokea malipo ya huduma zote na mafuta kupitia Airtel Money Tap Tap.
Airtel
Tanzania na Puma Energy Tanzania imezindua rasmi ushirikiano mpya ambao
unawawezesha wateja kulipia bidhaa na huduma zote za Puma Energy kwa
kutumia kadi ya “Airtel Money Tap Tap” kwenye vituo 46 nchini kote.
Ushirikiano
huu sasa utawawezesha wateja wa Airtel na Puma Energy kulipia mafuta na
bidhaa nyingine bila kutumia fedha taslimu bali watatumia kadi ya
Airtel Tap Tap ambayo imeunganishwa na akaunti zao za Airtel Money.
Huduma hii ni salama na rahisi kutumia inapatikana katika vituo vyote
vya Puma Energy nchi nzima, Huduma ya Airtel Money Tap Tap inatekelezwa
kwa awamu 2 ambapo awamu ya kwanza itahusu vituo vyote 20 vya Puma
jijini Dar es Salaam na awamu ya pili ni kwa ajili ya vituo vya mikoani
kuanzia mapema mwakani.
Akizungumza
wakati wa uzinduzi wa ushirikiano huo, Mkurugenzi Mkuu wa Airtel, Bwn
Sunil Colaso alisema “Sisi kama Airtel tunafuraha kuanzisha njia hii ya
malipo tukishirikiana na kampuni ya Puma Energy Tanzania. Ushirika huu
utaleta ushirikiano katika kutanua huduma zetu katika maeneo mengi zaidi
na kutoa usalama na uhakika wa huduma bora zaidi kwa wateja wote wa
Airtel na Puma Energy kwa masaa 24 na siku 7 za wiki
Tunaamini
kuwa ushirika huu na Puma Energy utaongeza ufanisi na kubadilisha
maisha ya jamii kuwa bora zaidi kwani wateja wetu wote wataweza kuzipata
huduma muhimu kwa urahisi kupitia kadi zao za Tap Tap” aliongezea
Colaso
Katika
hotuba yake, Meneja mkuu wa Puma Energy, Philippe Corsaletti
aliishukuru Airtel Tanzania kwa ushirika huo wa kibiashara na alieleza
imani yake katika ushirika huo akisema kwamba itaongeza thamani ya
biashara ya rejareja kwa kutoa fursa kwa watumiaji wa Airtel kutumia
vituo vya Puma Energy kama sehemu ya kulipia ununuzi wa mafuta na
vilainishi vya magari.
Alisema
Puma Energy itaendelea kufanya kazi na Airtel na kuhakikisha inapanua
upatikanaji wa huduma hii kwa vituo vyote vya mauzo vya Puma nchini
kote. Kufanikisha hili, Bwana Corsaletti aliitaka Airtel kupanua huduma
ya Tap Tap katika mikoa mingine nchini.
No comments:
Post a Comment