Rais
wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini TFF Jamal Malinzi wakikabidhiana
mkataba wa udhamini wa ligi kuu Vodacom na Mkuu wa Kitengo cha Fedha wa
DTB Joseph Musiba wenye thamani ya Milioni 250.
Mkuu
wa kitengo cha fedha wa benki ya DTB, Joseph Mabusi akizungumza na
waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati wa utiaji wa saini wa
mkataba wa udhamini wa ligi kuu Vodacom wenye thamani ya Milioni 250 kwa
msimu wa mwaka 2016/17,na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali pamoja na
viongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini Rais Jamali Malinzi.
Rais
wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini TFF Jamal Malinzi akitia saini
mkataba wa udhamini wa ligi kuu Vodacom wenye thamani ya Milioni 250
akiwa sambamba na Mkuu wa Kitengo cha Fedha wa Benki ya DTB Joseph
Mabusi ikishuhudiwa na waandishi wa wa habari na viongozi wengine wa
Bodi ya ligi pamoja na wawakilishi kutoka katika timu za ligi kuu.
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
SHIRIKISHO
la Mpira wa Miguu Nchini TFF limeingia mkataba wa mwaka mmoja wenye
thamani ya Milioni 250 na Benki ya Diamond Trust kwa ajili ya udhamini
wa ligii kuu ya Vodacom.
Mkataba
huo wa msimu wa mwaka 2016/17, DTB wanaungana na wadhamini wengine
ikiwa ni lengo la kuziwezesha timu hususani kwenye maendeleo ya soka
nchini.
Akizungumza
na waandishi wa habari katika hafla ya utiaji saini mkataba huo, Rais
wa TFF Jamali Malinzi amesema kuwa amezitaka taasisi nyingine kuiga
mfano huo kwani kwa kufanya hivyo kutawawezesha kukuza maendeleo ya soka
kwa timu za ligi kuu.
Malinzi
amesema kuwa, kuanzia sasa huduma zote za tiketi za kieletroniki
zitakuwa chini ya benki ya Diamond Trust kwa msimu wa 2016/2017.
Mkuu
wa Kitengo cha Fedha wa Benki ya DTB Joseph Mabusi amesema kuwa
udhamini huu utasaidia zaidi kukuza soka na pia wanajivunia kuwa sehemu
ya ligi kuu na wanaamini udhamini huu utazidisha ari ya kuwahudumia
watanzania wote.
Mabusi
amesema, mbali na kuidhamini ligi kuu Vodacom pia wanadhamini timu ya
ligi daraja la tatu Agathon iliyopo Mbagala na nia wadhamini wa michuano
ha Afrika Mashariki na Kati CECAFA Kagame Cup mwaka 2015.
Mkataba
huo utakuwa chachu ya maendeleo ya soka kwa nchi pamoja na kuzifanya
timu kujituma zaidi uwanjani pia unatarajiwa kuwa endelevu na kila mwaka
kutakuwa na mabadiliko mbalimbali kwenye mkataba huo.
No comments:
Post a Comment