Na Mwandishi Maalum, New York
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban
Ki Moon, amesema,
utashi wa kisiasa, matumizi
ya pato
la taifa na matumizi ya
fursa mbalimbali unaifanya Tanzania
kuwa moja ya nchi ya mfano katika uboreshaji
na upatikanaji wa elimu kwa wote.
Ban
Ki Moon ameyatamka hayo siku ya
jumapili, wakati wa hafla ya
uzinduzi wa Ripoti ya Kamisheni ya Kimataifa
kuhusu “ Kizazi kinachojifunza:
Uwekezaji katika elimu kwa dunia inayobadilika”.
Hafla
hiyo ilifanyika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa, na
kuhudhuriwa karibu na Makamishna wote
wanaounda tume hiyo akiwamo Rais Mstaafu
wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete.
Tume
hiyo ambayo ipo chini ya
uenyekiti wa Waziri Mkuu
Mstaafu wa Uingereza ambaye pia ni Mjuumbe Maalum wa Katika Mkuu wa Umoja wa Mataifa
kuhusu Elimu, inawahusisha pia baadhi ya Marais waliopo madakarani, Mawaziri
Wakuu waliopo madarakani na
waliostaafu, Mkurugenzi Mkuu wa
Benki ya Dunia, Mkurugenzi Mtendaji wa
UNESCO, Wawekaziji wakubwa akiwamo Bw. Aliko Dangote, Taasisi za utafiti, wataalamu wa masuala
ya fedha, asasi za kijamii na
makundi ya vijana wakiwamo wanafunzi.
“Uzoefu
wa nchi kama Tanzania, Vietnam na nchi yangu mwenyewe Korea, unaonyesha kwamba pale ambapo pana utashi
wa kisiasa, ukijumuishwa na uwepo wa
fursa na raslimali fedha kuna
kitu kinachowe kufanyika katika elimu.
Na kutokana na
uzoefu wa nchi kama Tanzania na
nyinginezo, Mkuu huyo wa Umoja wa
Mataifa amesema, Jumuiya ya Kimataifa ni lazima iwe tayari
kuzisaidia kwa mitaji nchi ambazo zimeamua na kujituma katika kuifanyia mageuzi
mifumo yake ya elimu na kujipati matokeo yanayoridhisha.
Jambo
kubwa
ambalo limetiliwa mkazo katika
ripoti hiyo ni uwekezaji wa raslimali fedha. Kwanza, kwa kila nchi
kukusanya kutumia mapato yake ya ndani, pili misaada kutoka
mashirika ya kimataifa na taasisi za
kimataifa, uwekezaji katika teknolijia
ya mawaliano hususani internent ili kutoa fursa kwa wanafunzi
kujipatia elimu
na maarifa zaidi nje ya masomo ya
darasani.
Akichangia
majadiliano ya uzinduzi wa ripoti hiyo, Rais
Mstaafu Jakaya Kikwete kama mmoja wa
Makamishna na ambaye pia aliongoza majadiliano kuhusu kipengele cha
tatu cha mapendekezo ya ripoti hiyo kuhusu ujumuishi katika elimu.
Kikwete alikuwa na haya ya kusema.
“Mafanikio
ya elimu lazimia yamfikie kila mmoja wakiwamo
wale wanaoishi katika mazingira
magugumu na wanaobaguliwa
wakiwamo wasichana”.
Akaongeza
kuwa bahati mbaya leo hii Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara msichana mmoja kati ya
ishirini wanaoishi katika maeneo
ya umaskini ndiyo walio katika hatua za kumaliza elimu ya msingi.
Rais
mstaafu Kikwete anaeleza kwamba takribani watoto
milioni 75 ambao wamo katika umri wa kwenda shule wanakabiliwa kila siku
na hatari moja ama nyingine. Idadi
hiyo inajumuisha watoto
milioni moja wa Syria ambao ni wakimbizi na ambao hawapati fursa ya kupata elimu.
“Kamisheni
hii inaweka visheni ya kuwapatia fursa vizazi vijavyo huku
mkazo ukitiliwa pia kwa
wakimbizi,watoto wa mitaani,wasichana,watoto walioko katika ajira na makundi
mengine ya jamii”. Akasema Rais mstaafu
Kikwete.
Kiwango
cha uwekezaji kinachotakiwa kuwekeza ni
kiasi cha dola trillion 3 ifikapo mwaka 2030. Aidha
kwa upande wa nchi ambazo uchumi wake ni mdogo zinatakiwa kuwekeza kutoka asilimia tatu
ya pato lake hadi kufikia asilimia tano ya pato la taifa, wakati zile
zenye uchumi wa kati zitatakiwa
kuwekeza kutoka kiwango cha
asilimia tano ya sasa hadi kufikia
asilimia 5.7.
Ili malengo hayo ya uwekezaji yaweze
kufikiwa, Makamishna kupitia ripoti yao wanatoa wito kwa Mawaziri wa Fedha
kushirikiana na kufanya kati kwa karibu na
Viongozi wao wakuu wa serikali.
Hata
hivyo imeelezwa pia kupitia ripoti hiyo
kwamba uwekezaji wa raslimali fedha si
kigezo pekee cha kuwapatia
fursa ya elimu kila mtoto mwenye umri wa kwenda shule.
Bali
kinachotakiwa pia ni uwekezaji
tangu mtoto anapokuwa tumboni kwa maana ya mzazi kupata lishe bora na huduma bora za afya, mtoto anapozaliwa kupata
fursa ya lishe na makuzi bora, kuwa na fursa ya kupata elimu
ya awali ambayo watafiti wanasema ni
jambo la msingi sana katika kumuandaa mtoto.
Vile
vile makamishna wamesisitiza haja na
umuhimu wa walimu kuwa sehemu ya mabadiliko ya sekta ya elimu kwa
wao wenyewe kupatiwa mafunzo ya mara kwa mara, kupewa motisha ya
kutekeleza majukumu yao na kuachwa watekeleze
kazi ya ufundishaji pasipo kuingiliwa au kuongezewa majukumu mengine ambayo
yapo nje ya kazi yao ya ualimu.
Makamishna
wanatahadharisha kupitia ripoti
hiyo kwamba kama serikali hazitafanya haraka kuwekeza raslimali fesha katika elimu, watoto katika nchi zenye
pato dogo la kiuchumi wataendelea
kubaki katika dimbwi la umaskini huku wakiwa hawa ujuzi wala
maarifa ya aina yoyote ile.
Ripoti
inabainisha
zaidi kwamba “ zaidi ya theruthi mbili ya watoto wenye umri wa kwenda
shule katika nchi zenye kipato cha chini hawataweza kupata maarifa na
elimu ya msingi ifikapo 2030 licha ya malengo ambayo jumuiya ya
kiataifa imejiwekea ya kuhakikisha
kila mtoto anakwenda shule”
Inaarifiwa kupitia
ripoti hiyo kwamba ni nusu
tu ya watoto wote wenye
umri wa kwenda shule ya msingi na zaidi kidogo ya robo ya wanafunzi wa sekondari
katika nchi zenye ukuaji mdogo wa
uchumi au zile zenye uchumi wa kati ndio
wanaopata fursa ya kujifunza maarifa/ ujuzi wa awali.
Vile
vile ripoti hiyo imebaini pia kuwa
watoto 330 milioni walioko katika shule
za msingi na sekondari wanamaliza elimu
yao wakiwa hawajaelimika.
No comments:
Post a Comment