Matukio/Kimataifa :Briana Kagemuro azidi kung'ara. Anyakuwa kombe laTennis USTA L6 -Mid Atlantic - Wazalendo 25 Blog

Breaking

Glory to Story.


Post Top Ad


14 Sep 2016

Matukio/Kimataifa :Briana Kagemuro azidi kung'ara. Anyakuwa kombe laTennis USTA L6 -Mid Atlantic


Mchezaji tennis Briana Kagemuro mwishoni mwa juma alishinda katika michuano ya shirikisho la Tennis Marekani (USTA) Mid Atlantic, kwa upande wa wasichana walio chini ya miaka 12 (12 and under) a yaliyofanyika katika viwanja vya Bullis Potomac -Maryland.
Mashindano hayo yalijumuisha wasichana nane ambapo Kage Briana alifanikiwa kumbwaga mpinzani wake Emory Wilson katika fainali kwa seti 6-4,6-3.

KageBriana akiwa na kombe lake pamoja na mshindi wa pili Emory Wilson
Wakati huohuo yalifanyika mashindano ya mix doubles ambapo KageBriana na kakaye Mwombeki walichukuwa ushindi wa tatu kwa michuano ya vijana wa umri wa miaka 14 (14 and under yaliyofanyika Potomac Maryland.
Bryan na Briana wakiwa na medali zao

Post Top Ad