Matukio : Watumishi wawili Ardhi wafukuzwa kazi huku wengine wawili wakipewa onyo - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


12 Sept 2016

Matukio : Watumishi wawili Ardhi wafukuzwa kazi huku wengine wawili wakipewa onyo

 Isaac Joseph akihutubia moja ya mikutano Huko Monduli: Picha na Mkataba

Na Vero Ignatus wa Wazalendo 25 Blog, Monduli
Baraza la madiwani  Halmashauri ya Monduli limewafukuza kazi watumishi wawili na wawili kupewa onyo kali huku baraza hilo likiridhia mwanasheria wa Halmashauri hiyo kurejea kazini baada ya kushinda kesi

Akiwataja watumishi hao Mwenyakiti wa baraza la madiwani isack Joseph Kopriano ameeleza kuwa wamejadiliana kwamuda mrefu kuhusiana na watumishi hao na ndipo wakafikia maamuzi ya kuwafukuza kazi Mrasimu ramani Leonard Mkwave pamoja na Afisa ardhi mteule Kitundu Mkumbo,waliopewa.baraua za onyo ni  Mkuu wa idara ya ardhi ndugu Adili Mwanga pamoja na Afisa ardhi mpimaji Leonard Haule huku baraza hilo likiridhia mkuu wa kitengo cha sheria Gidion Kamara akirudishwa  kazini baada ya kushinda kesi iliyokuwa ikimkabili.
Hatua hiyo imetokana watumishi waliofukuzwa kazi baada ya kukutwa na makosa mawili kila mmoja hali iliyopelekea baraza kuchukua uamuzi wa kuwafuta kazi,ambapo wenzao wawili makosa yao hao walipewa onyo kali.

Kwa upande wa mwanasheria alifikishwa mahakamani na Takukuru lakini aliweza kushinda kesi hiyo na kukosa kuwa na tuhuma ambazo zilizokuwa zinamkabili hivyo bataza likaridhia kumrudisha kazini.

Kwa upande wake mkurugenzi wa halmashauri hiyo Stephen  Ulaya amesema kuwa atayafanyia kazi maagizo aliyopewa na mkuu wa wilaya bila kumuonea mtu aibu wala kumpendelea wala kumuonea mtu na ataongoza halmashauri kwa kufuata kanuni na taratibu.

Aidha Mkurugenzi huyo amewataka watumishi hususani watendaji wa vijiji na
kata kuhakikisha wanafuata taratibu na kanuni kwa kuitisha mikutano ya wananchi kwa wakati na yeyote atakayebainika kwenda kinyume na hilo sheria itafuata mkondo wake.

Hata hivyo amewataka madiwani kuwapa ushirikiano watumishi hao vitongoji vijiji na kata ambao wamekuwa wakifanya kazi kwa mazowea ili kuhakikisha wananchi wanapata hudumakwa wakati na kutoa michango yao kwaajili ya maendeleo ya wilaya hiyo.

"Monduli ni yetu sote lazima tufanye kazi kwa bidii kuhakikisha wananchi wanapata hudumakwa wakati, na sintamuonea haya mtu wala aibu,mtumishi yeyote atakayekiuka sheria za utumishi ,ili kuhakikisha maendeleo.yanawafikia wananchi kwa wakati, alisisitiza ulaya"

Alibainisha kuwa yeyote atakayekutwa miradi yamaendeleo ipo chini yakiwango na wanango na amabaye hatafanya mkutano mkuu wa wa wananchi katika kitongoji,kikijina kata kwa wakati hatakuwa amejiondoa mwenyewe.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad