Mwenyekiti
wa wadau wa barabara Tanzania Eng. Abdul Awadhi (Kushoto) akizungumza
na Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya
Ujenzi) Eng .Joseph Nyamhanga (Kulia) wakati wa mkutano wa Saba wa
wadau wa miundombinu ya reli na barabara,jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti
wa wadau wa barabara Tanzania Eng. Abdul Awadhi akiongea na wadau wa
miundombinu ya barabara na reli wakati wa mkutano wa Saba wa wadau
hao, uliofanyika jijini Dar es salaam.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akiongea na
wadau wa miundombinu ya barabara na reli wakati wa mkutano wa Saba wa
wadau hao, uliofanyika jijini Dar es salaam.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa(Wa pili
kutoka kulia) akijadiliana na wadau wa miundombinu ya barabara na reli
mara baada ya kufungua mkutano huo.Kulia kwake ni Katibu Mkuu Wizara wa
Wizara hiyo (Sekta ya Ujenzi) Eng .Joseph Nyamhanga.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akikagua
ramani inayonyesha miundombinu ya barabara nchini wakati wa uzinduzi wa
mkutano wa saba wa sekta ya Miundombinu ya barabara na reli, jijini Dar
es salaam.
Picha na Benjamin Sawe-Maelezo
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa amewataka
wadau wa sekta ya miundombinu ya Reli na Barabara kushirikiana na
Serikali katika kuchangamkia fursa za utekelezaji wa miradi mbalimbali
ya sekta hiyo hapa nchini.
Akizungumza
jijini Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Kimataifa wa Saba
wa wadau wa Sekta hiyo, Prof. Mbarawa amesema kwa sasa Serikali kupitia
Rais wa Awamu ya Tano inatekeleza miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa
bomba la mafuta kutoka Tanga hadi nchini Uganda, ujenzi wa barabara ya
kulipia wa Dar es Salaam-Chalinze KM 144 (Dar-Chalinze Express way) na
ujenzi wa reli ya kati hivyo ni muhimu kwa wadau hao kutumia mkutano huo
katika kuijadili miradi hiyo.
“Ni
matumaini yangu katika mkutano huu mtajadili kwa pamoja namna ya
kushirikiana na Serikali katika kutekeleza fursa za ujenzi wa
miundombinu hapa nchini ikiwemo kuungana na Serikali (Public Private
Partnership) au kwa njia nyingine yoyote”, amesema Waziri Mbarawa.
Amesisitiza
wadau hao kuja kwa wingi nchini na kuwekeza katika sekta hiyo ili
kupanua ushindani wa kibiashara katika soko la kitaifa na kimataifa.
Waziri
Mbarawa amebainisha kuwa Serikali inaendelea kutafuta pesa kutoka kwa
wadau mbalimbali na kushirikisha taasisi binafsi kupitia mpango wa
kushirikiana baina ya Serikali na Taasisi hizo (Public Private
Partnership) ili kutekeleza miradi ya miundombinu ya reli na barabara
nchini.
Kwa
Upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Reli ya Tanzania na
Zambia (TAZARA) Eng. Bruno Ching’andu amesema kuwa licha ya TAZARA kuwa
na treni za umma zinazotoa huduma za usafiri nchini bado inakabiliwa na
changamoto nyingi ikiwemo uhaba wa fedha katika uendeshaji wa shirika
hilo ikiwemo gharama za ujenzi na ukararabati wa mabehewa.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
No comments:
Post a Comment