Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Madini,
Profesa James Mdoe (Katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa
Japan nchini, Masaharu Yoshida (Wa pili kutoka kulia), Kaimu Kamishna wa
Madini, Mhandisi Ally Samaje (Wa kwanza kushoto), Watendaji kutoka
Serikali ya Japan na JOGMEC wakati wa semina iliyolenga katika
uendelezaji endelevu wa rasilimali madini nchini.
Meneja
wa Kanzidata na Uchakataji wa Taarifa za Jiolojia kutoka Wakala wa
Jiolojia (GST), Terence Ngole akizungumza wakati wa Semina iliyoandaliwa
na Shirika la Umma kutoka Japan linalojishughulisha na Mafuta, Gesi na
Metali (JOGMEC), Wizara ya Uchumi, Biashara na Viwanda ya Japan, Wakala
wa Jiolojia Tanzania (GST), pamoja na Wizara ya Nishati na Madini
iliyofanyika jijini Dar es Salaam iliyolenga katika uendelezaji Endelevu
wa Rasilimali Madini nchini.
Balozi
wa Japan nchini, Masaharu Yoshida (wa kwanza kulia) akimsikiliza Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Madini,
Profesa James Mdoe (hayupo pichani) akifungua Semina iliyoandaliwa na
Shirika la Umma kutoka Japan linalojishughulisha na Mafuta, Gesi na
Metali (JOGMEC), Wizara ya Uchumi, Biashara na Viwanda ya Japan, Wakala
wa Jiolojia Tanzania (GST), pamoja na Wizara ya Nishati na Madini
iliyofanyika jijini Dar es Salaam iliyolenga katika uendelezaji Endelevu
wa Rasilimali Madini nchini.
Wadau
mbalimbali waliohudhuria Semina iliyoandaliwa na Shirika la Umma kutoka
Japan linalojishughulisha na Mafuta, Gesi na Metali (JOGMEC), Wizara ya
Uchumi, Biashara na Viwanda ya Japan, Wakala wa Jiolojia Tanzania
(GST), pamoja na Wizara ya Nishati na Madini iliyofanyika jijini Dar es
Salaam iliyolenga katika uendelezaji Endelevu wa Rasilimali Madini
nchini.
Wadau
mbalimbali waliohudhuria Semina iliyoandaliwa na Shirika la Umma kutoka
Japan linalojishughulisha na Mafuta, Gesi na Metali (JOGMEC), Wizara ya
Uchumi, Biashara na Viwanda ya Japan, Wakala wa Jiolojia Tanzania
(GST), pamoja na Wizara ya Nishati na Madini iliyofanyika jijini Dar es
Salaam iliyolenga katika uendelezaji Endelevu wa Rasilimali Madini
nchini.
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Madini,
Profesa James Mdoe akifungua Semina iliyoandaliwa na Shirika la Umma
kutoka Japan linalojishughulisha na Mafuta, Gesi na Metali (JOGMEC),
Wizara ya Uchumi, Biashara na Viwanda ya Japan, Wakala wa Jiolojia
Tanzania (GST), pamoja na Wizara ya Nishati na Madini iliyofanyika
jijini Dar es Salaam iliyolenga katika uendelezaji Endelevu wa
Rasilimali Madini nchini.
Teresia Mhagama na Devotha Myombe
Tanzania
imeahidi kuendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji katika Sekta ya
Madini kama ilivyoainishwa katika Sera ya Madini ya mwaka 2009.
Hayo
yameelezwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa
James Mdoe wakati wa semina iliyoandaliwa na Shirika la Umma kutoka
Japan linalojishughulisha na Mafuta, Gesi na Metali (JOGMEC), Wizara ya
Uchumi, Biashara na Viwanda ya Japan, Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST),
pamoja na Wizara ya Nishati na Madini iliyofanyika jijini Dar es Salaam
iliyolenga katika uendelezaji endelevu wa rasilimali madini nchini.
Alisema
kuwa, Dira ya Maendeleo ya Mwaka 2025 imelenga katika kuanzisha migodi
mikubwa, ya kati na midogo inayoendeshwa kwa kuzingatia usalama na
utunzaji wa mazingira hivyo mazingira mazuri ya uwekezaji yatavutia
wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kuwekeza ili kuendeleza Sekta ya
Madini nchini.
Profesa
Mdoe alisema kuwa semina hiyo ililenga katika kupata taarifa
zilizohuishwa kutoka Japan na Tanzania kuhusu shughuli za utafiti na
utunzaji wa mazingira katika Sekta ya Madini nchini na kujadiliana juu
ya kuendeleza ushirikiano kati ya nchi husika.
“Semina
hii ni muhimu kwani Taasisi hizi zitajadiliana kuhusu kuendeleza
ushirikiano katika sekta hii, kufahamu fursa za uwekezaji kwenye Sekta
ya Madini kwani wadau kutoka Tanzania na Japan wataweza kupata taarifa
za utafiti kuhusu madini yaliyopo nchini na pia Taasisi ya JOGMEC
itapata fursa ya kueleza shughuli zake barani Afrika,” alisema Profesa
Mdoe.
Akieleza
kuhusu Sekta ya Madini nchini, Profesa Mdoe alisema kuwa Sekta hiyo kwa
sasa inachangia asilimia 3.5 katika Pato la Taifa na kueleza kuwa
asilimia hiyo bado ni ndogo kwani lengo la Serikali ni kuona kuwa Sekta
hiyo inachangia mpaka asilimia 10 kufikia mwaka 2025.
Hata
hivyo Profesa Mdoe alisema kuwa ili sekta hiyo ichangie ipasavyo katika
Uchumi wa Taifa, kutategemea kutoshuka kwa bei ya bidhaa zinazotokana
rasilimali madini na uchumi wa dunia kuendelea kukua ili makampuni
yanayojishughulisha na utafiti na uchimbaji wa madini yapate fedha
kutoka Taasisi za kifedha duniani ili kuanzisha shughuli za utafiti na
uchimbaji wa madini.
Aidha
Profesa Mdoe aliwaalika wawekezaji kujenga vituo vitakavyotumika katika
shughuli za uongezaji thamani madini ya Tanzania kwani alisema kuwa
uongezaji thamani madini ndani ya nchi utasaidia kuongeza ajira kwa
wananchi, ubadilishanaji wa teknolojia kutoka nchi zilizobobea katika
shughuli hizo na kuwezesha ukusanyaji wa kodi ambayo itasaidia katika
shughuli nyingine za maendeleo.
Awali
Meneja wa Kanzidata na Uchakataji wa Taarifa za Jiolojia kutoka GST,
Terence Ngole, alieleza JOGMEC na GST walisaini Mkataba wa Makubaliano
mwaka 2010 ambapo mashirikiano kati ya Taasisi hizo yamesaidia kuongeza
utaalam na teknolojia katika utafiti wa madini kupitia mafunzo
mbalimbali ya muda mrefu na mfupi yanayotolewa na Shirika la JOGMEC.
Alisema
kuwa Semina hiyo imeshirikisha wadau mbalimbali kutoka Japan na
Tanzania ambao wanajishughulisha na Sekta ya Madini na Mazingira na
kwamba ni semina ya kwanza kuendeshwa nchini na Shirika la JOGMEC.
No comments:
Post a Comment