----------------------------------------------------
Serikali
imeahidi kuwasaidia wazalishaji wadogo wa bidhaa mbalimbali zikiwemo
bidhaa za ngozi kwa kuwajengea uwezo wa kuzalisha bidhaa nyingi na
bidhaa bora, ili wazalishaji hao wageuke ni viwanda vidogo, ili uchumi
wa Tanzania ya Viwanda, viwanda hivyoviwe vinamilikiwa na Watanzania
wakiwemo wazalishaji wadogo wa bidhaa mbalimbali.
Ahadi hiyo imetolewa leo na Katibu Mkuu, Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Prof Adolf Mkenda kwenye mkutano wa wazalishaji wa bidhaa za ngozi uliokwenda sambamba na maonyesho ya siku moja ya bidhaa za ngozi nchini yaliofanyika leo kwenye Viwanja wa Maonyesho ya Saba Saba, vya Mwl. J.K.Nyerere, Barabara ya Kilwa, Dar es Salaam.
Ahadi hiyo imetolewa leo na Katibu Mkuu, Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Prof Adolf Mkenda kwenye mkutano wa wazalishaji wa bidhaa za ngozi uliokwenda sambamba na maonyesho ya siku moja ya bidhaa za ngozi nchini yaliofanyika leo kwenye Viwanja wa Maonyesho ya Saba Saba, vya Mwl. J.K.Nyerere, Barabara ya Kilwa, Dar es Salaam.
Prof.
Mkenda amesema , serikali ya awamu ya tano ina nia ya dhati ya
kuwawezesha Watanzania kuumiliki uchumi wa taifa kwa kuweka mazingira
wezeshi na vivutio mbalimbali na masharti nafuu kwa Watanzania kushiriki
katika Tanzania ya Viwanda, ila ametoa changamoto kwa wazalishaji hao
kuunganisha nguvu zao kwa pamoja na kuunda viwanda vidogo vidogo hivyo
kuwa rahisi kusaidiwa kwa pamoja kuliko mmoja mmoja.
Prof.
Mkenda amesema “Serikali inavipaumbele vya kuwawezesha wazawa kuanzisha
viwanda ili kukuza bidhaa za Tanzania ikiwemo bidhaa za sekta za ngozi,
hivyo mnapaswa kuwa na ujasiri wa kuzalisha na kutumia fursa hiyo kwa
ajili ya ushindani”
Pia
alitumia muda huo kuwahamasisha wazalishaji hao kutumia soko la pamoja
la jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) pamoja na soko la SADC maana
wanahaki ya kuuza kwenye kanda hizo. Na aliwaasa kutumia taasisi zingine
za serikali zinazoweza kuwainua kwenye sekta hiyo ili kuondokana na
changamoto mbalimbali watambue kuwa serikali inajipanga kukomesha bidhaa
za mtumba nchini ili kuboresha soko la bidhaa bora zinazozalishwa
katika nchi yetu.
Prof.
Mkenda alimalizia kwa kutoa changamoto kwa Mamlaka ya Biashara
Tanzania, kuandaa maonyesho mbalimbali yakiwemo maonyesho ya kisekta,
ili viwanja vya maonyesho vya Saba Saba vitumike wakati wote wa mwaka
mzima kwa maonyesho mbalimbali, na sio kipindi cha Saba Saba tuu mpaka
Saba Saba nyingine, na kutoa vito kwa Tantrade kutoa maeneo ya kudumu
kwa wajasiliamali na wazalishaji wadogo wadogo wapate maeneo rasmi ya
kuonyesha bidhaa zao wakati wote.
Naye kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), Edwin
Rutageruka akijibu changamoto za Katibu Mkuu, amesema kwa kuanzia,
TanTrade ipo tayari kuwapa mafunzo ya ujasiliamali ya namna
watakavyoweza kupenya kwenye masoko mbalimbali ili kukuza sekta hiyo ya
ngozi, na kutenga eneo maalum kwa wazalishaji wadogo wadogo wa bidhaa
mbalimbali na wajasiliamali kuonyesha bidhaa zao na pia kuanza mchakato
wa kuutumia uwanja wa maoyesho ya Saba Saba kuendeshea magulio ya masoko
ya Jumamosi na Jumapili, (Saturday Market na Sunday Market).
Mwenyekiti wa chama cha wazalishaji wa bidhaa za ngozi (TALEPPA)Dedan Munisi, amesisitiza
sasa umefika wakati kwa Watanzania sio tuu kwa kuonyesha uzalendo wa
kuthamini bidhaa za ndani, bali kuzinunua na kuzitumia bidhaa
zinazozalishwa na Watanzania wenyewe, na kuwataka kuacha kasumba ya
kudharau chako nan kuthamini cha mwenzio kwa kutukuza bidhaa za nje kwa
kudhani zina ubora zaidi kuliko zile zinazolishwa nchini, na kusisitiza
bidhaa za ngozi zinazozalishwa nchini zina ubora wa hali ya juu kuliko
bidhaa za nje.
Kwa
upande wao, Wazalishaji hao wakiongozwa na Denis D. Kileo mzalishaji wa
bidhaa za ngozi kutoka Woiso Original Products alisema changamoto kubwa
ni watanzania kutoweza kutofautisha viatu vya ngozi bandia kutoka nje
ya nchi vyenye ufanano na bei kuwa chini hivyo sekta hiyo kudumaa ni
wakati sasa wauzaji wa maduka mbalimbali nchini kuwaamini wazalishaji
na bidhaa za sekta ya ngozi na kuvipeleka mbele sokoni bidhaa zao ili
kupanua masoko.
Naye
Bi. Cecilia China mtafiti kutoka TIRDO aliwashauri wazalishaji wa
bidhaa za ngozi kutumia taasisi za serikali za kisayansi nchini ili
kuondokana na changamoto mbalimbali zinazowakabili kwenye sekta hiyo ili
kupunguza gharama kwenye uzalishaji wa bidhaa zao na waweze kushauriwa
kitaalam njia bora ya uzalishaji wenye kukidhi soko la ndani na nje ya
nchi.
Mamlaka
ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tantrade) (TanTrade) ikishirikiana
na na Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji wameandaa mkutano huo wa
wazalishaji wa bidhaa za ngozi kwa lengo la kuwakutanisha wadau wa
serikali na sekta binafsi ili kujadili fursa, changamoto na mikakati ya
kuendeleza sekta hiyo ambayo inamchango mkubwa uchumi wa taifa kuelekea
kenye Tanzania ya viwanda.
No comments:
Post a Comment