Matukio : Rais Dk. Magufuli aongoza mkutano wa 17 wa dharura wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki ,Jijini Dar - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Friday, 9 September 2016

Matukio : Rais Dk. Magufuli aongoza mkutano wa 17 wa dharura wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki ,Jijini Dar

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais Dkt John Pombe Magufuli na viongozi wenzie wakisimama wakati wimbo wa Jumuiya ukipigwa wakati  wa ufunguzi wa Mkutano wa 17 wa Dharura wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki katika ukumbi wa mikutano wa Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 8, 2016

Sehemu ya waliohudhuria wakiwa wamesimama wakati wimbo wa Jumuiya ukipigwa wakati  wa ufunguzi wa Mkutano wa 17 wa Dharura wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki katika ukumbi wa mikutano wa Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 8, 2016


Ujumbe wa Burundi
Sehemu ya mabalozi wa nchi mbalimbali wakiwa mkutanoni hapo
Wageni kutoka nchi wanachama
Mabalozi wa nchi mbalimbali wakiwa mkutanoni hapo
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais Dkt John Pombe Magufuli  akiongoza mkutano. Anafuatiwa na Rais Paul Kagame wa Rwanda, Mwakilishi maalum wa Rais wa Sudan ya Kusini Mhe Aggrey Tisa Sabuni, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Balozi Liberat Mfumukeko

Waziri Mkuu Mstafu Jaji Joseph Sinde Warioba (kati) na Katibu Mkuu Mstaafu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Balozi Juma Mwapachu (kushoto) wakiwa na viongozi wastaafu wa Jumuiya
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais Dkt John Pombe Magufuli  akiongoza mkutano. Kushoto kwake ni  Rais Paul Kagame wa Rwanda, Mwakilishi wa Rais wa Sudan ya Kusini Mhe Aggrey Tisa Sabuni, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein. Kulia kwake ni Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda, Naibu Rais wa Kenya Mhe William Rutto na mwakilishi wa Rais wa Burundi na Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo  Balozi Alain Aime Nyamitwe

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais Dkt John Pombe Magufuli  akiongoza mkutano akiwa na Rais Paul Kagame wa Rwanda na Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais Dkt John Pombe Magufuli akijadiliana jambo na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Balozi Liberat Mfumukeko

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais Dkt John Pombe Magufuli akihutubia mkutano huo

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais Dkt John Pombe Magufuli akiendelea na hotuba yake

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais Dkt John Pombe Magufuli akipigiwa makofi na wahudhuriaji

Sehemu ya mabalozi wakisikiliza hotuba ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais Dkt John Pombe Magufuli 

Wanahabari  wakirekodi  hotuba ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais Dkt John Pombe Magufuli 


Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais Dkt John Pombe Magufuli akihutubia

Dkt Mussa Lulandala wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam alikuwa nyota wa mkutano kwa kuweza kufasiri kwa ustadi wa hali ya juu hotuba zote kutoka Kiingereza kwenda Kiswahili na Kiswahili kwenda Kiingereza
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein akiteta jambo na Balozi Liberat Mfumukeko

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais Dkt John Pombe Magufuli  akiongea jambo na Rais Paul Kagame

Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (atayesimamia Utawala na Fedha) Mhe. Christophe Bazivamo akila kiapo katika mkutano huo.
Naibu Katibu Mkuu wa Jumjuiya ya Afrika Mashariki (atayesimamia Utawala na Fedha) Mhe Christophe Bazivamo akitoa heshima meza kuu baada ya kula  kiapo katika mkutano huo.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais Dkt John Pombe Magufuli  akimpongeza Naibu Katibu Mkuu wa Jumjuiya ya Afrika Mashariki (atayesimamia Utawala na Fedha) Mhe Christophe Bazivamo baada ya kula kiapo katika mkutano huo.

Rais Paul Kagame wa Rwanda  akimpongeza Naibu Katibu Mkuu wa Jumjuiya ya Afrika Mashariki (atayesimamia Utawala na Fedha) Mhe Christophe Bazivamo baada ya kula kiapo katika mkutano huo.

Naibu Rais wa Kenya Mhe William Rutto  akimpongeza Naibu Katibu Mkuu wa Jumjuiya ya Afrika Mashariki (atayesimamia Utawala na Fedha) Mhe Christophe Bazivamo baada ya kula kiapo katika mkutano huo.

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein akimpongeza Naibu Katibu Mkuu wa Jumjuiya ya Afrika Mashariki (atayesimamia Utawala na Fedha) Mhe Christophe Bazivamo baada ya kula kiapo katika mkutano huo.

Viongozi na wabunge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakimshangilia Naibu Katibu Mkuu wa Jumjuiya ya Afrika Mashariki (atayesimamia Utawala na Fedha) Mhe Christophe Bazivamo baada ya kula kiapo katika mkutano huo.
Viongozi na wabunge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakimpongeza  Naibu Katibu Mkuu wa Jumjuiya ya Afrika Mashariki (atayesimamia Utawala na Fedha) Mhe Christophe Bazivamo baada ya kula kiapo katika mkutano huo.
Manaibu Makatibu wakuu wa  Jumuiya ya Afrika Mashariki wakimpongeza Naibu Katibu Mkuu mpya wa Jumjuiya ya Afrika Mashariki (atayesimamia Utawala na Fedha) Mhe Christophe Bazivamo baada ya kula kiapo katika mkutano huo.
Sehemu ya waliohudhuria
Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda akihutubia
Rais Paul Kagame wa Rwanda akiongea machache
Naibu Rais wa Kenya Mhe William Rutto akizungumza machache
Naibu Rais wa Kenya Mhe William Rutto akisisitiza jambo
 mwakilishi wa Rais wa Burundi na Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo  Balozi Alain Aime Nyamitwe akiongea machache

Mwakilishi wa Rais wa Sudan ya Kusini Mhe Aggrey Tisa Sabuni akishukuru kwa nchi yake kukubaliwa kuwa mwanachama kamili wa Jumuiya

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein akiongea machache ikiwa ni pamoja na kukumbushia umuhimu wa Sudan ya Kusini kuwa mwanachama wa Jumuiya kwani awali nchi hiyo ilikuwa kiungo muhimu kwa nchi wanachama

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein akiendelea kuhutubia

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein akisisitiza jambo

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Balozi Liberat Mfumukeko akisoma maazimio ya mkutano

Meza kuu wakisaini na kuridhia maazimio ya mkutano 
Wimbo wa Jumuiya ukipigwa kuashiria mwisho wa mkutano
Wageni mashuhuri wakisimama kwa wimbo wa Jumuiya
Viongozi wakisalimiana na waalikwa
Viongozi katika picha ya pamoja na mawaziri kutoka nchi wanachama
Viongozi katika picha ya pamoja na mawaziri kutoka nchi wanachama
Viongozi katika picha ya pamoja na wabunge wa Jumuiya hiyo 
Picha ya pamoja na Sekretarieti ya Jumuiya
Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu Bw. Gerson Msigwa akisimamia shughuli ya picha za pamoja
Viongozi na wageni mashuhuri
Viongozi na wageni mashuhuri
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais Dkt John Pombe Magufuli  akimsindikiza Rais Paul Kagame wa Rwanda

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais Dkt John Pombe Magufuli akiteta jambo na Naibu Rais wa Kenya Mhe William Rutto

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais Dkt John Pombe Magufuli akiteta jambo na Naibu Rais wa Kenya Mhe William Rutto

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais Dkt John Pombe Magufuli akiagana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na mmoja wa wageni baada ya kumalizika kwa mkutano huo.

Ujumbe wa Tanzania kwenye mkutano huo

No comments:

Post a Comment