Meneja
Masoko wa DKT international Tanzania Sialouise Shayo akizungumza na
wageni mbalimbali waliofika kujionea Kliniki mpya na ya kisasa
iliyozinduliwa katika makao makuu ya Shirika hilo hivi karibuni Masaki,
jijini Dar es salaam kwa ajili ya Afya ya uzazi kwa kina mama.
Meneja
Mradi wa programu ya Trust community maternity homes kutoka DKT
International Tanzania Carol Francis Mango akifafanua jambo kwa
waandishi wa habari katika hafla ya uzinduzi wa kliniki hizo mpya
zilizotengenezwa maalumu kwaajili ya kukidhi mahitaji ya afya ya uzazi
na uzazi wa mpango kwa wanawake wanaoishi kwenye miji midogo katika
jamii yetu. Uzinduzi wa kliniki hizo ulifanyika jana katika makao makuu
ya Shirika hilo jijini Dar es salaam.
Mkunga
kutoka DKT International Tanzania Adella Hugo akizungumza na waandishi
wa habari kuhusiana na huduma mbalimbali zinazopatikana kwenye Kliniki
mpya ya uzazi wa Mpango iliyozinduliwa jana katika Makao makuu ya
Shirika hilo Masaki, jijini Dar es salaam. Kliniki hiyo ni maalumu
kwaajili ya kukidhi mahitaji ya afya ya uzazi na uzazi wa mpango.
Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika la DKT International Tanzania Raphael da Silva
akizungumza na vyombo mbalimbali vya habari wakati wa hafla ya uzinduzi
wa Kliniki mpya za Shirika hilo zijulikanazo kama “Trust community
maternity homes”. Kliniki hizo mpya ni maalumu kwa ajili ya kukidhi
mahitaji ya afya ya uzazi na uzazi wa mpango kwa wanawake wanaoishi
kwenye miji midogo katika jamii yetu. Uzinduzi huo ulifanyika jana
katika Makao makuu ya Shirika hilo Masaki, jijini Dar es salaam.
Meneja
Masoko wa DKT International Tanzania Sialouise Shayo akionyesha baadhi
ya bidhaa kwa waandishi wa habari zinazopatikana kwenye Kliniki mpya ya
uzazi wa Mpango iliyozinduliwa jana katika Makao makuu ya Shirika hilo
Masaki, jijini Dar es salaam. Kliniki hiyo ni maalumu kwaajili ya
kukidhi mahitaji ya afya ya uzazi na uzazi wa mpango.
SHIRIKA
lisilo la kiserikali la DKT International Tanzania limezindua mfano wa
Kliniki mpya ziitwazo “Trust community maternity homes kwa ajili ya
wananchi wa kipato cha kawaida zinazoendeshwa na wakunga mbalimbali.
“Trust
Community Maternity Homes” – Ni kliniki zinazojitosheleza
zilizotengenezwa kwa ubunifu kwa kutumia kontena ya kusafirishia mizigo,
kliniki hizi zimetengenezwa maalumu kwaajili ya kukidhi mahitaji ya
afya ya uzazi na uzazi wa mpango kwa wanawake wanaoishi kwenye miji
midogo katika jamii yetu.
Kiliniki
za “Trust Community Maternity Homes” zilizinduliwa kwa umma wakati wa
uzinduzi wa kliniki ya “Trust Health & Wellness Clinic “ ya Dar Es
Salaam na ofisi mpya za DKT International Tanzania mnamo tarehe mbili
September, 2016
“Kila
mwaka, wanawake milioni moja hapa Tanzania ambao hawakukusudia kupata
ujauzito hupata ujauzito” alisema mkurugenzi mkuu wa DKT international,
Raphael da Silva.
“Hali
hii si tu kuwa ina athiri wanawake hawa kifedha, afya zao binafsi na
hali ya kiuchumi ya familia zao, lakini pia zinapelekea kuongeza uhitaji
wa Serikali kutoa huduma za kiafya pamoja na elimu kwa watoto hawa
.Kama tunaweza kufanikisha kutoa huduma zenye ubora wa hali ya juu za
afya ya uzazi na uzazi wa mpango kwa jamii katika miji midogo na
wanajamii ambao hawapati huduma hizi kiurahisi, tutafanikiwa kuleta
mabadiliko chanya katika maisha ya wanawake hawa” alisema.
“Trust
Community Maternity Homes ni kliniki zinazojitosheleza ndani ya kontena
la kusafirishia mizigo, zinazoendeshwa na wakunga wataalamu na wenye
uzoefu wa muda mrefu kama washirika chini ya kliniki mama za “Trust
health and wellness clinics” . Alisema meneja mradi, Karoli Mango.
“Kliniki
hizi zinatoa ubora ule ule wa huduma , usiri na msaada sawa sawa na
Kliniki zetu nyingine za Trust zinazopatikana mikoani hapa nchini
.Kliniki yetu ya kwanza ya “ Trust community maternity homes” ya mjini
Kahama iko katika hatua za mwisho za maandalizi kabla ya ufunguzi”
aliongeza.
Trust
ina mpango wa kuingia mikataba yenye masharti mepesi na wakunga wazoefu
ambayo itawawezesha kukodisha na baadae kuzi miliki kliniki hizi.
Wakunga wanaotoa huduma hizi watatumia kliniki hizi ambazo ziko ndani
ya kontena ambazo zinatumia umeme wa sola , zenye uwezo wa kutoa huduma
kamili za afya ya uzazi na uzazi wa mpango, pamoja na huduma nyingine za
afya kwa jamii. Wakunga hawa watajipatia kipato kwa kutoza kiasi kidogo
cha fedha kwa huduma na bidhaa zitakazo tolewa katika kliniki hizi.
Kwa
sasa , kuna “ Trust health and wellness clinic” nne ambazo ziko Dar
es Salaam, Dodoma, Mbeya and Mwanza na pia kuna kliniki na hospitali
washirika 30 ambazo zinatoa huduma kwa kutumia chapa ya Trust.
Kliniki ya Msasani peninsula ya Dar Es Salaam ilifunguliwa mapema mwezi Julai.
No comments:
Post a Comment