Maisha : Wajasiriamali watakiwa kujikita katika ufugaji wa Kuku - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


7 Sept 2016

Maisha : Wajasiriamali watakiwa kujikita katika ufugaji wa Kuku


Na Ferdinand Shayo wa Wazalendo 25 Blog ,Arusha.

Wajasiriamali nchini wametakiwa kujikita katika Ufugaji wa kuku wa Kienyeji na kisasa ili waweze kunufaika kiuchumi kufuatia ongezeko la uhitaji mkubwa wa mayai na nyama katika maeneo ya mengi hususan kwa wafanyabiashara wa vyakula.

Hayo yameelezwa na Mjasiriamali Boniventura Shiyo anayejihusisha na ufugaji huo amesema kuwa kwa sasa biashara hiyo imemuongezea kipato ambacho anakitumia kujiletea maendeleo pamoja na kuendesha familia pasipo kuyumba.

Mjasiriamali huyo amewataka Watanzania kujenga tabia ya uthubutu kwani soko la biashara ya kuku ni kubwa na linazidi kukua kila kukicha.

Hata hivyo Boniventura amesema kuwa kwa sasa anatumuia mashine maalumu ya inayototoa mayai na kuwa vifaranga maarufu kama incubator ambayo imemuongezea fursa ya kuwa muuzaji wa vifaranga pia.

Biashara ya ufugaji wa kuku ni moja kati ya biashara zinazoshamiri kwa kasi katika maeneo mingi nchini hususan maeneo ya mijini ambapo ndipo masoko makubwa yanapatikana kutokana na idadi kubwa ya watumiaji wa bidhaa za mayai na nyama ya kuku.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad