Michezo : Mashindano EAC yaanza Kigali, Tanzania yashika nafasi ya tatu Ridha - Wazalendo 25 Blog

Breaking

Glory to Story.


Post Top Ad


10 Aug 2016

Michezo : Mashindano EAC yaanza Kigali, Tanzania yashika nafasi ya tatu Ridha


Wanamichezo wa Tanzania Mashariki wakiingia Uwanjani wakati wa Ufunguzi wa Michuano hiyo  uliofanyika katika Uwanja wa Amahoro Kigali Nchini Rwanda Picha na

 Wanamichezo wa Michezo ya majeshi kwa Nchi za Afrika Mashariki wakiingia Uwanjani wakati wa Ufunguzi wa Michuano hiyo  uliofanyika katika Uwanja wa Amahoro Kigali Nchini Rwanda 

Baadhi ya maofisa na Wanamichezo wa Michezo ya majeshi kwa Nchi za Afrika Mashariki wakifuatilia Ufunguzi wa Michuano hiyo  uliofanyika katika Uwanja wa Amahoro Kigali Nchini Rwanda 

Baadhi ya maofisa na Wanamichezo wa Michezo ya majeshi kwa Nchi za Afrika Mashariki wakifuatilia Ufunguzi wa Michuano hiyo  uliofanyika katika Uwanja wa Amahoro Kigali Nchini Rwanda 

Baadhi ya Askari wa JWTZ  wakifuatilia Ufunguzi wa Michuano ya majeshi kwa Nchi za Afrika mashariki uliofanyika katika Uwanja wa Amahoro Kigali Nchini Rwanda.

 Waziri wa Ulinzi wa Rwanda Jenerali James kabarebe (wa pili Kulia) akifuatilia jambo wakati wa ufunguzi wa Michuano ya majeshi kwa nchi za Afrika mashariki katika Uwanja wa Amahoro Kigali nchini Rwanda

Wanarianda walioshiriki mashindano ya majeshi  kwa nchi za Afrika mashariki wakichuana wakati wa Mashindano hayo kwa Mbio za nyika Wanawake ambapo Tanzania imeshika nafasi ya Tatu.

(picha na Selemani Semunyu)

Na Seleamani Semunyu JWTZ.

MASHINDANO ya majeshi kwa Nchi za Afrika mashariki yameingia Siku yake ya kwanza baada ya kuzinduliwa huku Tanzania ikishika nafasi ya tatu katika Riadha kwa wanawake  katika mbio zilizokuwa na Ushindani Mkali na kufanyika katika Uwanja wa APRC Kicukiro. .

Mtanzania Catherine Lange aliiwezesha Timu ya JWTZ kuibuka na Ushindi wa tatu huku kwa Wanaume Mwanariadha Fabiano  Nelson kufanya vyema licha kukosa ushindi wa jumla kutokana na kuwa peke yake mbele nyuma ya wakenya waliochukua ushindi wa Kwanza.  

Awali akifungua mashindano hayo Waziri wa Ulinzi wa Rwanda Jenerali James Kabarebe amewapongeza Wakuu wa Majeshi  Kutoka Nchi za Afrika Mashariki kwa kuendeleza michezo na kutoa nafasi kwa nchi zo kushiriki katika mashindano ya Afrika Mashariki ambayo yamekuwa kiungo katika kuimarisha Ushirikiano.

Aliyasema hayo leo wakati akizindua wa michezo hiyo katika Sherehe zilizofanyika katika Uwanja wa Amahoro Kigali Nchini Rwanda na Kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Majeshi kutoka majeshi ya Nchi  Nne zinazoshiriki Michuano hiyo.

“ Michezo ni Sehemu ya Majukumu ya Jeshi Lakini nawapongeza na kuyapa uzito mashindano haya kwani yamekuwa yakitusaidia katika kuimarisha ushirikiano wa Nchi hizo ili kuhakikishia inaendelea kuwa sehemu salama.

Waziri Jenerali Kabarege alitoa Wito kwa Wakuu hao kutumia nafasi ya Michezo hii kufanyia kazi changamoto kama zipo zinazokabili majeshi katika ukanda huu.

Awali Mkuu wa majeshi wa Rwanda Jenerali Patrick Nyamvumba  aliwahahakikishia Wanamichezo maandalizi Mazuri na kuwataka kuwa huru na kuchanganyika na Wanyarwanda ambao alidai wameajiandaa kuwapokea.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Mkuu wa majeshi ya Ulinzi wa Tanzania ambaye ni Mkuu wa mafunzo na Utendaji Kivita Meja Jenerali Issa Nassoro amesema anamatumaini makubwa kwa Timu za Tanzania kurejea na vikombe.

Post Top Ad