Matukio : Ummy Mwalimu atoa wito kwa wananchi kutoa ushirikiano Mapitio ya Sera ya Afya. - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Monday, 22 August 2016

Matukio : Ummy Mwalimu atoa wito kwa wananchi kutoa ushirikiano Mapitio ya Sera ya Afya.





 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akitoa ufafanuzi kuhusu masuala mbalimbali ya wizara anayoiongoza alipokutana na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam. 
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akitoa wito kwa wananchi kushirikiana na wataalam wanaofanya  Mapitio ya Sera ya Afya kutoka Chuo kikuu cha Dar es Salaam, Chuo cha Afya Muhimbili na Wataalam wa Ofisi mbalimbali za Serikali zinazojishughulisha na masuala ya utekelezaji wa Sera ya Afya ya mwaka 2007.

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO
TAARIFA KWA UMMA.

MAPITIO YA SERA YA AFYA YA MWAKA 2007.
Utoaji wa huduma za afya nchini una simamiwa na Sera ya Afya ya mwaka 2007. Dhumuni kuu la Sera hii ya Afya ya Mwaka2007, ni kuinua hali ya afya ya wananchi wote na hasa wale walioko kwenye hatari zaidi, kwa kuweka mfumo wa huduma za Afya utakaokidhi mahitaji ya wananchi na kuongeza umri wa kuishi wa Watanzania. Mpaka sasa, Wizara yangu inaendelea kutekeleza Sera hii katika kusimamia utoaji na upatikanaji wa huduma za afya nchini. Katika utekelezaji wa Sera hii, Wizara na Sekta ya Afya kwa ujumla imepata mafanikio mbalimbali. Mafanikio haya ni pamoja na:

  • Ongezeko la Vituo vya kutolea Huduma: Wizara imeendelea kuboresha huduma za tiba kwa kutekeleza Mpango wa Maendeleo wa Afya ya Msingi (MMAM). Katika utekelezaji wa Mpango huo,vituo vya kutolea huduma za afya vimeongezeka kutoka vituo 5,172 mwaka 2005 hadi 7,247 mwaka 2015, sawa na ongezeko la vituo 2,075. Kati ya vituo vyote vilivyopo nchini, Vituo 5,072 ni vya Serikali na 2,175 nivyataasisibinafsi.

  • Kupunguza vifo vya watoto chini ya miaka mitano kutoka112 kwa kila vizazi hai 1000 mwaka 2005 hadi 81 kwa vizazi hai 1000 mwaka 2010. Aidha, Taarifa ya Kimataifa ya Septemba 2013, imeonesha kuwa Tanzania tumeweza kufikia Lengo la millennia namba 5, la angalau kuwa na vifo 54 kwa kila vizazi hai 1000, Tanzania iliweza kufikia lengo hilo kabla ya mwaka 2015..

  • VifovitokanavyonamatatizoyaUzazivimepunguakutoka 578 kwakilavizazihai 100,000 mwaka 2005 hadivifo 432 kwavizazihai 100,000 mwaka 2012 navifo 410 kwavizazihai 100,000 mwaka 2014. PiamatumiziyaUzaziwampangoyameongezekakutokaasilimia 20 mwaka 2005 hadiasilimia 27 mwaka 2010.

  •   Huduma za Chanjo: Serikali imefanikiwa katika kupanua wigo wa huduma za chanjo ambapo, kiwango cha chanjo kimeongezeka kutoka asilimia 90 mwaka 2005 hadi asilimia 97 mwaka 2014. Kutokana na mafanikio katika chanjo, Wizara imefikia viwango vya kimataifa vya kutokomeza pepopunda kwa watoto wachanga mwaka 2012 na pia imeweza kudhibiti ugonjwa wa Polio.
  •   Katika kipindi hiki cha kutekeleza sera hii, Wizara imeanzisha huduma mpya za kibingwa na uchunguzi hapa nchini na kuwawezesha wananchi kupata huduma za kibingwa ambazo awali zilikuwa hazitolewi hapa nchini. Huduma hizo ni pamoja na upasuaji mkubwa wa moyo, upasuaji wa mifupa,mishipa ya fahamu na ubongo, kusafisha damu kwa wagonjwa wenye matatizo ya figo na uanzishaji wa huduma za dharura.

  •   Udhibiti wa Malaria: kiwango cha maambukizi ya malaria kimeshuka kutoka asilimia 18 mwaka 2008 na kufikia asilimia 10 mwaka 2012 (THMIS).
  •   Udhibiti wa UKIMWISerikali imepata mafanikio katika kudhibiti UKIMWI, kiwango cha maambukizi ya Virusi vya UKIMWI(VVU) kimepungua kutoka asilimia 7 mwaka 2004 hadi kufikia asilimia 5.1 mwaka 2011/12. Vituo vya tiba kwa watu wanaoishi na VVU vimeongezeka kutoka 91 mwaka 2005 hadi 1,463 mwaka 2015. Hadi Juni 2015, jumla ya watu 703,589 wanapatiwa ARV ikilinganishwa na Mwaka 2005, ambapo watu wanaoishi na VVU 16,199 walipatiwa huduma hii.


 Pamoja mafanikio mbalimbali yaliyopatika katika utekelezaji wa Sera hii, Sekta ya Afya imekuwa na changamoto mbalimbali na kusababisha madhumuni ya Sera kutofikiwa. Changamoto hizo ni pamoja na:
  1.   Upungufu wa vifaa, vifaa tiba na vitendanishi pamoja na dawa katika vituo vya kutolea huduma za Afya,
  2.  Uhaba wa miundombinu ya kutolea huduma za afya nchini hasa, zahanati, vituo vya afya na hospitali,
  3.  Uwezo mdogo wa viwanda vinavyozalisha dawa hapa nchini,
  4.    Upungufu mkubwa wa watumishi wa Afya katika ngazi zote za kutolea huduma
  5.  Maendeleo madogo ya upunguzaji wa Vifo vya wakinamama vinavyotokana na Ujauzito.
  6.    Maendeleo na mabadiliko ya tabia na mwenendo wa maisha vimebadili sura ya magonjwa. Aidha, hali hii imesababisha kuanza kujitokeza kwa magonjwa ya kuambukiza na yasiyo ya kuambukiza na yanayotokana na ajali na majanga, ambayo kwa huduma zilizopo haziwezi kukidhi.
  7.  Kuendelea kupungua kwa Rasilimali fedha katika  Sekta ya Afya na kusababisha kuendelea kushuka kwa ubora wa huduma za afya katika vituo vya kutolea huduma.
  8.  Kuwalinda wananchi hasa wenye kipato cha chini katika katika kupata huduma za afya wakati wanazihitaji.

  1. Uwepo wa vituo vya kutosha vya kutolea huduma na kudumisha upatikanaji wa huduma bora za afya katika vituo vya afya.
  2. Ongezeko la idadi ya watu ambalo linapelekea ongezeko la mahitaji ya huduma za afya.
Aidha, changamoto hizo na Mabadiliko mbalimbali ambayo yatatokea yamepelekea serikali kutoa maagizo na kutayarisha mikakati mbali mbali ya Serikali kwa lengo la kuboresha huduma zitolewazo kwa umma. Mikakati na maagizo hayo ni pamoja:

  • Utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Nne wa Sekta ya Afya 2015-2020 ( HSSP IV)
  • Utekelezaji wa Mkakati wa Ugharamiaji wa Huduma za Afya
  • Utekelezaji katika mfumo wa malipo kwa matokeo.
  • Mpango wa Serikali wa matokeo makubwa sasa
  • Mabadiliko ya Sayansi na Teknolojia, inayobadilisha namna huduma za Afya      zinavyotolewa
  • Ongezeko la Magonjwa sugu, hasa magonjwa ambayo siyo ya kuambukiza ambayo yana gharama kubwa na yanaweza kuzuilika.
  Mpango wa Serikali wa matokeo makubwa sasa

   Mabadiliko ya Sayansi na Teknolojia, inayobadilisha namna huduma za Afya zinavyotolewa
  Ongezeko la Magonjwa sugu, hasa magonjwa ambayo siyo ya kuambukiza ambayo yana gharama kubwa na yanaweza kuzuilika.

Kutokana na changamoto zilizojitokeza na utekelezaji wa mikakati na maagizo hayo , ni muhimu kufanya mapitio ya Sera ya Afya ya mwaka 2007 ili utekelezaji wa matamko ya kukidhi  Lengo na  Madhumuni yaliyokusudiwa kufikiwa na Sera.

Mapitio haya, yanafanywa na Wizara yangu kwa kushirikiana na Chuo kikuu cha Dar es Salaam, Chuo cha Afya Muhimbili na Wataalam wa Ofisi mbalimbali za Serikali zinazojishughulisha na masuala ya utekelezaji wa Sera ya Afya ya mwaka 2007.

Nawaomba wananchi wote kutoa ushirikiano wakutosha kwa Wizara na Wataalam wa timu hii katika kuhakikisha kuwa mnatoa maoni yenu kwa uwazi kwa ajili ya kusaidia maendeleo a Sekta ya Afya nchini. 

Wananchi wote mnaweza kutoa maoni yenu kupiti Tovuti ya Wizara (www.moh.go.tz) au kuwasilisha maoni yenu pia Kupitia anuanimaoni.sera@moh.go.tz. Mwisho wa kutoa maoni ni tarehe 30 Oktoba 2016.

Nawashukuru sana.

Ummy A. Mwalimu (mb)
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto

No comments:

Post a Comment