Matukio : Rais Dk. Magufuli Amuapisha Mrisho Gambo kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha , Ikulu Jijini Dar - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


19 Aug 2016

Matukio : Rais Dk. Magufuli Amuapisha Mrisho Gambo kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha , Ikulu Jijini Dar


  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Mrisho Gambo kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha Ikulu jijini Dar es Salaam.


 Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa pamoja na Mkuu mpya wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo mara baada ya tukio la Kiapo Ikulu jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi wa kwanza (kulia) na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Tawala za mikoa  na Serikali za Mitaa TAMISEMI Selemani Jafo wa kwanza (kushoto).
 Rais Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo mara baada ya kumuapisha Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akimpongeza Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo mara baada ya kuapishwa Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha Rais Mstaafu wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Donald Kaberuka aliyefika Ikulu kwa ajili ya mazungumzo.
 Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Rais Mstaafu wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Donald Kaberuka mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam. Picha na IKULU.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad