Kaimu
Mkurugenzi wa Afya ya Uzazi na Mtoto kutoka Wizara ya Afya na Ustawi
za Jamii,Dk.Georgina Msemo akiongea na wafanyakazi wa Vodacom na wazazi
wenye watoto wanaotibiwa saratani (Hawapo pichani) wakati wa hafla ya
Vodacom Tanzania Foundation kukabidhi msaada wa shilingi milioni 20 kwa
ajili ya kusaidia watoto wenye saratani wanaoendelea na matibabu katika
hospitali ya Muhimbili,(kushoto) ni Mkuu wa Vodacom Foundation Tanzania
Renatus Rwehikiza na (kulia) ni Mkurugenzi wa Shirika lisilo la
kiserikali linaloshugulika na matibabu ya watoto wenye saratani la
Tumaini la Maisha,Dk Trish Scanlan.
Mkuu
wa Vodacom Tanzania Foundation, Renatus Rwehikiza akiongea na vyombo
vya habari muda mfupi baada ya kukabidhi msaada wa kusaidia watoto
wanaotibiwa ugonjwa wa Saratani katika hospitali ya
Muhimbili.Wafanyakazi wa Vodacom pia walitoa msaada wa fedha
taslimu,vyakula na vitu mbalimbali vya kuwasaidia ambapo pia walitenga
muda wao kusafisha maeneo ya hosteliwanazoishi watoto hao na walishiriki
kuwatengenezea lishe na kucheza nao kwa ajili ya kuwapatia faraja.
Wafanyakazi
wa Vodacom Tanzania katika picha ya pamoja muda mfupi baada ya
kushiriki katika kazi za kijamii za kusafisha mazingira ya hosteli
wanazoishi watoto wanaotibiwa Saratani katika hospitali ya Muhimbili
ambapo pia waliwatengenezea lishe na kucheza nao,vilevile walijitolea
fedha zao kununua mahitaji mbalimbali ya watoto hao.
Baadhi
ya wafanyakazi wa Vodacom wakishiriki kusafisha mazingira ya hosteli
wanazoishi watoto wanaotibiwa Saratani katika hospitali ya Muhimbili
Mkuu
wa Vodacom Foundation Tanzania Renatus Rwehikiza na (kulia) akiongea na
wafanyakazi wa Vodacom na wazazi wenye watoto wanaotibiwa saratani
(Hawapo pichani) wakati wa hafla ya Vodacom Tanzania Foundation
kukabidhi msaada wa shilingi milioni 20 kwa ajili ya kusaidia watoto
wenye saratani wanaoendelea na matibabu katika hospitali ya Muhimbili
(katikati) ni Kaimu Mkurugenzi wa Afya ya Uzazi na Mtoto kutoka Wizara
ya Afya na Ustawi za Jamii,Dk.Georgina Msemo na kulia ni Mkurugenzi wa
Shirika lisilo la kiserikali linaloshugulika na matibabu ya watoto
wenye saratani la Tumaini la Maisha,Dk Trish Scanlan
Mkurugenzi
wa Shirika lisilo la kiserikali linaloshugulika na matibabu ya watoto
wenye saratani la Tumaini la Maisha,Dk Trish Scanlan (Kulia) akiongea na
wafanyakazi wa Vodacom na wazazi wenye watoto wanaotibiwa saratani
(Hawapo pichani) wakati wa hafla ya Vodacom Tanzania Foundation
kukabidhi msaada wa shilingi milioni 20 kwa ajili ya kusaidia watoto
wenye saratani wanaoendelea na matibabu katika hospitali ya Muhimbili
(katikati) ni Kaimu Mkurugenzi wa Afya ya Uzazi na Mtoto kutoka Wizara
ya Afya na Ustawi za Jamii,Dk.Georgina Msemo na (kushoto ) ni Mkuu wa
Vodacom Foundation Tanzania Renatus Rwehikiza.
Mkurugenzi
wa Shirika lisilo la kiserikali linaloshugulika na matibabu ya watoto
wenye saratani la Tumaini la Maisha,Dk Trish Scanlan (Kulia) akipokea
baadhi ya vifaa vilivyotolewa na wafanyakazi wa Vodacom kutoka kwa Mkuu
wa Vodacom Foundation Tanzania Renatus Rwehikiza (wa nne kutoka kulia)
wengine pichani wanaoshuhudia ni Kaimu Mkurugenzi wa Afya ya Uzazi na
Mtoto kutoka Wizara ya Afya na Ustawi za Jamii,Dk.Georgina Msemo (Wa
tatu kutoka kushoto).Wengine ni maofisa wa Vodacom na wazazi wenye
watoto wanaosumbuliwa na Saratani.
.Baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom wakicheza na watoto.
Baadhi
ya wafanyakazi wa Vodacom wakishiriki kutengeneza lishe wakati
walipojitolea muda wao kusaidia watoto wahanga wa ugonjwa wa Saratani
wanaoendelea na matibabu katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Watoto
wanaosumbuliwa na maradhi ya saratani ambao wanaendelea kupata matibabu
katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili wamepatiwa msaada wa milioni 20
kutoka taasisi ya Vodacom Tanzania kwa ajili ya kufanikisha matibabu
yao na kuwapatia lishe bora.
Mbali
na msaada wa fedha wafanyakazi wa kampuni ya Vodacom Tanzania wametenga
muda wao kushiriki kusafisha maeneo ya hosteli wanaoishi watoto hao
ikiwemo kucheza nao,kuwatengenezea lishe pia wametoa msaada wa vyakula
na fedha taslimu kwa ajili ya kusaidia matibabu ya watoto hawa.
Msaada
huo umetolewa leo katika hosteli wanazoishi watoto hao zilizopo
katika hospitali ya Taifa Muhimbili kupitia Shirika lisilo la
kiserikali linalojishughulisha na kuwahudumia watoto wenye maradhi ya
Saratani linalojulikana kama Tumaini la Maisha ambapo mgeni rasmi
alikuwa ni Kaimu Mkurugenzi wa Afya ya Uzazi na Mtoto kutoka Wizara ya
Afya na Ustawi za Jamii,Dk.Georgina Msemo.
Akitoa
pongezi kwa niaba ya serikali,Dk.Msemo amesema kuwa serikali
inafarijika inapoona makampuni ya biashara kama Vodacom yanajitoa
kusaidia jitihada za serikali za kukabiliana na changamoto mbalimbali
hususani katika sekta ya afya ambako kunahitajika uokoaji wa maisha ya
watu.
“Nawapongeza
sana wafanyakazi wa Vodacom na taasisi yake yake ya kusaidia masuala
ya kijamii ya Vodacom Tanzania Foundation pia nimefurahishwa kuona
wafanyakazi mmejitoa kuchangia kusaidia watoto hawa wenye matatizo ya
saratani na kutenga muda wenu kuja kusafisha mazingira eneo hili
wanaloishi,kushiriki kuwatengenezea lishe na kujumuika nao kwa kucheza
nao kwa ajili a kuwapatia faraja”.Alisema.
Akiongea
wakati wa kupokea msaada huo Mkurugenzi wa Shirika la Tumaini la
Maisha,Dk. Trish Scanlan alishukuru kwa msaada huo kutoka Vodacom
Tanzania Foundation kwa watoto utakaowafikia na kuwanufaisha walengwa
kupitia shirika hilo lisilo la kiserikali linaloshughulika na
kuwasaidia watoto wahanga wa ugonjwa wa Saratani wanaotibiwa katika
hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Alisema
kuna idadi kubwa ya watoto zaidi ya 300 wanaolazwa hospitalini hapo
wakiwa wanakabiliwa na saratani ya aina mbalimbali na kutokana na umri
wao na wanahitaji misaada ya madawa ya kuwatibu ikiwemo lishe bora na
mahitaji mengine mengi ya kila siku.
Kwa
upande wake Mkuu wa Vodacom Tanzania Foundation,Renatus Rwehikiza
alisema kuwa siku zote taasisi hiyo itakuwa mstari wa mbele kuunga mkono
jitihada za serikali katika kusaidia jamii hususani katika nyanja za
Afya na Elimu.
“Afya
ni moja ya suala ambalo tunalipa kipaumbele na ndio maana tumekuwa
tukivalia njuga kutokomeza magonjwa mbalimbali mojawapo ikiwa ugonjwa
huu wa saratani ambao siku hadi siku umekuwa ukiongezeka na kusababisha
vifo vya watu wengi ”Alisema.
Alisema
Vodacom Foundation imetoa kiasi cha shilingi milioni 20 kupitia taasisi
ya Tumaini la Maisha ili kuwawezesha watoto hawa kupatiwa madawa,lishe
bora na mahitaji mbalimbali hususani katika kipindi hiki kigumu
wanachoendelea kupata matibabu na aliwataka wadau wengine kujitokeza
kusaidia wenye matatizo mbalimbali kwenye jamii.
Mmoja
wa wazazi ambaye mtoto wake anaendelea na matibabu ya Saratani Grace
Nyambisu kutoka mkoani Dodoma akiongea kwa niaba ya wenzake alishukuru
Vodacom Tanzania Fondation kwa msaada huu muhimu wa lishe na madawa kwa
watoto wao katika kipindi hiki kigumu ambacho wanaendelea kupata
matibabu.
Alisema
kwa msaada huo taasisi hiyo imethibitisha usemi wa akufaaye kwa dhiki
ndiye rafiki kwa kuwa umetolewa katika muda mwafaka ambao watoto
wanahitaji kupata lishe bora na madawa wakati huohuo wazazi wengi wakiwa
wanakabiliwa na changamoto ya kutomudu kuwahudumia kutokana na
kukabiliwa na ugumu wa maisha ambao unasababishwa na kutumia muda wao
mwingi kuuguza watoto badala ya kujishughulisha na kazi za uzalishaji
kwa ajili ya kuwaingizia vipato.
No comments:
Post a Comment