Mwezi Julai umeshuhudia fainali za kombe la soka Ulaya (Euro 2016), michuano ya Tennis uwanja maarufu wa Wimbledon na matamasha mbalimbali za fasihi, ambapo mwandishi wa habari hizi alihudhuria kuiwakilisha Tanzania kwa ngoma. Wakati kilio cha ugaidi na mauaji vikitafuna kama chawa, Marekani , Ufaransa na Uturuki, London palifanyika maandamano ya takriban wakazi milioni moja wakipiga kelele maisha magumu na aghali .... Kipya Knyemi, ukumbi wa SOAS, London, 7 Julai. Balozi mpya wa Uingereza,Tanzania Bi Sarah Cooke na Mheshimiwa Dk Asha-Rose Migiro aliyechukua nafasi ya Mhe. Peter Kallaghe. Mkurugenzi wa Kituo cha Biashara , Ubalozi Tanzania, London, Bw Yusufu Kashangwa na Balozi Dk Asha Rose Migiro na mabalozi wa Uingereza, Bi Sarah Cooke (wa pili ) na mstaafu Dianna Melrose, ndani ya tafrija hiyo ya BTS, chuo cha lugha SOAS, London. Maandamano ya wananchi na vyama vya upinzani yaliyofanyika Jumamosi 16 Julai, London , kushutumu hali ngumu na kufunga mkanda (“austerity”) inayozidi kuwadhalilisha maskini na wafanyakazi wa kawaida, Ulaya. Picha ya Twitter Janet Chapman (kulia) mwanaharakati na mwanachama wa BTS ambaye muda mrefu amepigania haki za wasichana na wanawake wanaokeketwa Tanzania akizungumza na Adjoa Ajimadu, toka Ghana katika tafrija hii ya mabalozi wapya SOAS. Bango la tamasha maarufu la kimataifa la Ledbury, Uingereza lililoshirikisha miaka 400 ya maisha ya mwandishi nguli William Shakespeare. Tanzania iliwakilishwa na mwandishi wenu. Bi Hope Katanga, Mtanzania na Julian Marcus na mkewe, wanachama waaminifu wa Jumuiya hii ya Waingereza na Watanzania. Dk Andrew Coulson, (kulia) mhadhiri wa chuo kikuu cha Birmingham, aliyesimamia shughuli ya kuwakaribisha mabalozi. Hapa anazungumza na askari aliyepigana vita vya pili vya dunia, Kapteni David Nichol. Kapteni Nichol aliyewahi pia kuwa mkuu wa mkoa mmoja, Tanganyika enzi za ukoloni , ana umri wa miaka 95 na huitembelea Tanzania mara kwa mara na mkewe. Mwandishi na mwanamuziki Freddy Macha baada ya kutumbuiza ngoma tamasha la fasihi la Wabangladesh, London.
Balozi Dk Asha- Rose Migiro akisalimiana na Bw Alistair Scott wa kampuni ya mafuta ya Ophir Energy inayotazamia kujihusisha kikamilifu na madini hayo Tanzania. Wataalamu kadhaa wa Ophir Energy walihudhuria hafla hii ya SOAS.
No comments:
Post a Comment