Matukio : Wadau nchini waaswa kishirikiana na serikali kusaidia Kambi za Wazee - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633


PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0676 643 633

Friday, 29 July 2016

Matukio : Wadau nchini waaswa kishirikiana na serikali kusaidia Kambi za Wazee


Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga imeziasa Taasisi binafsi, Makampuni, Asasi za Kiraia na watu binafsi kushirikiana na katika kutatua changamoto zinazokabili makazi ya wazee na watu wenye ulemavu nchini. 

Akiongea wakati alipotembelea Makazi ya kulea wazee na watu wenye ulemavu ya Kolandoto leo Mkoani Shinyanga Bi. Sihaba amesema kuwa ametembelea baadhi ya makazi hayo na kuona yanahitaji msaada mkubwa hasa ujenzi wa nyumba za malazi, umeme na madawa hivyo Taasisi binafsi, Makampuni, Asasi za Kiraia na watu binafsi hawana budi kushirikiana na serikali kamaliza kabisa changamoto hizo.

“nimetembelea makazi kadhaa sasa, changamoto ni nyingi, wazee hawa wanahitaji msaada mkubwa sana hivyo kwa nafasi hii natoa wito kwa Taasisi binafsi, Makampuni, Asasi za Kiraia na watu binafsi kushirikiana na serikali katika kuziondoa changamoto hizi katika makazi haya ili kuweza kuwafanya wazee hawa kufurahia maisha katika makazi haya”.Amesema Bi. Sihaba.

Naye Afisa Mfawidhi wa Makazi ya Kulea Wazee ya Kolandoto Bi.Sophia Kang’ombe amewaomba wahisani na serikali kwa ujumla kusaidia katika ukarabati na ujenzi wa majengo katika makazi hayo ili kupunguza changamoto ikiwemo uvamizi wa vijana wanaotumia vilevi na bangi kuingia katika nyumba hizo na kutishia kuwafanyia vitendo vibaya wazee wenye jinsia ya kike.

Akizungumza kwa niaba ya Wazee katika Makazi ya Kolandoto Mkoani Shinyanga Mzee Samora Maganga amesema kuwa kituo hicho kwa kiasi fulani kipo katika hali nzuri ila wanaiomba serikali iwasaidie katika kutatua changamoto ya umeme na majengo kwani imekuwa kero ya muda mrefu sasa.

Aidha Bi. Sihaba akiongea na Wazee katika Makazi ya Amani Mkoani Tabora aliwapongeza walezi wa makazi hayo kwa kuamua kutoa kadi za matibabu za CHF kwa wazee hao na kushauri Walezi wa Makazi mengine ya Wazee nchini kuiga mfano huo ili kusaidia katika utoaji bora wa huduma za afya kwa wazee.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga akisalimiana na wazee alipotembelea Makazi ya kulea wazee ya Kolandoto leo Mkoani Shinyanga.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga akisaini kitabu cha wageni alipofika katika Makazi ya Kulea Wazee ya Kolandoto leo Mkoani Shinyanga.Kulia ni Mkurugenzi Idara ya Ununuzi na Ugavi kutoka Wizara hiyo Bw. Richard Mallya.

Afisa Mfawidhi wa Makazi ya Kulea Wazee ya Kolandoto Bi.Sophia Kang’ombe akimkabidhi taarifa ya kituo hicho Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga wazee alipotembelea Mkazi hayo leo Mkoani Shinyanga.

Afisa Mfawidhi wa Makazi ya Kulea Wazee ya Kolandoto Bi.Sophia Kang’ombe akimuleza Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga (kulia) changamoto za Makazi hayo na kumuomba kusaidia kusimamia utatuliwaji wa matatizo hayo ikiwemo ujenzi wa majengo kwa ajili ya malazi ya wazee hao, Katikati ni Afisa Maendeleo ya Jamii kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Amina.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga akiongea na Wazee wanaoishi katika Makazi ya Kulea Wazee ya Kolandoto leo Mkoani Shinyanga na kuwahakikishia serikali kuendelea kuwasaidia kutatua changamoto zinazowakabili ili kuwawezesha kuishi katika mazingira rafiki. Katikati ni Afisa Maendeleo ya Jamii kutoka Wizara hiyo Bi. Amina… na kushoto ni Afisa Mfawidhi wa Makazi ya Kulea Wazee ya Kolandoto Bi.Sophia Kang’ombe.

Afisa Mfawidhi wa Makazi ya Kulea Wazee ya Kolandoto Bi.Sophia Kang’ombe akimuonesha Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga sehemu ya nyumba zinazohitaji ujenzi kwa ajili ya Makazi ya Wazee hao. Wakati wa Ziara ya Kutembelea Makazi ya Wazee na kuona hali halisi ya makazi hao.

Sehemu ya Nyumba kwa ajili ya Makazi ya Wazee ambazo hazitumiki kutokana na kuwa katika hali mbaya katika Makazi ya kulea Wazee ya Kolandoto Mkoani Shinyanga.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga akizungumza na Mzee Samora Maganga ambaye ni Mwenyekiti wa Wazee katika Makazi ya kulea Wazee ya Kolandoto Mkoani Shinyanga.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga akisalimiana na Wazee katika Makazi ya Kulea Wazee ya Amani leo Mkoani Tabora.

Mganga Mkuu wa Manispaa ya Tabora Dkt. Rashidi Said Akisoma taarifa ya kituo cha Makazi ya kulea wazee ya Amani yaliyopo Mkoani Tabora kwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga alipotembelea kituo hicho leo Mkoani Tabora ambapo mbali na changamoto zinazokabili kituo hicho pia wamefanikiwa kutoa kadi za Matibabu ya Afya za CHF kwa wazee wote kituoni hapo.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkingaakimpa Zawadi ya Sabuni Mwenyekiti wa Kijiji cha Kolandoto Bw. George Busambilo kwa niaba ya Wazee katika Makazi hayo.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga akikagua Nyumba Wazoishi Wazee katika Mkazi ya Wazee ya Amani leo Mkoani Tabora.Picha zote na Hassan Silayo-MAELEZO

No comments:

Post a Comment