Katibu
Mkuu Kiongozi Mstaafu Balozi Ombeni Sefue akizungumza na Menejimenti ya
Wakala wa Taifa wa Utafiti wa Nyumba Bora na Vifaa vya Ujenzi na Vifaa
vya Ujenzi (NHBRA) wakati alipofanya ziara katika taasisi hiyo mwishoni
mwa wiki ili kujionea shughuli mbali mbali zinazofanywa na taasisi
hiyo , Kwa kiwango kikubwa (NHBRA) imeonyesha ni taasisi inayoweza
kujenga nyumba za bei nafuu sana hasa vijijini ili watanzania wa maeneo
hayo waweze kupata makazi bora ya kuishi kwa bei rahisi zaidi, Kulia
katika picha ni Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo Bw.Matiko Samson
Mturi.
Taasisi
hiyo pia imekuwa ikijihusisha na mafunzo teknolojia ya ujenzi wa
nyumba za bei nafuu kwa vikundi mbalimbali nchini ikiwa ni pamoja na
kuwafundisha juu ya utengenezaji wa matofali, vigae vya kuezekea nyumba
pamoja na ujenzi wa nyumba za zenyewe ambapo taasisi na wananchi
mbalimbali wanaweza kufaidika na mpango huo nchini.Mkurugenzi
Mtendaji wa taasisi hiyo Bw.Matiko Samson Mturi akizungmza wakati
alipokuwa akimkaribisha Balozi Ombeni Sefue wakati alipotembelea katika
taasisi ya Wakala wa Taifa wa Utafiti wa Nyumba na Vifaa vya Ujenzi
NHBRA Mwenge jijini Dar es salaam.
Bw.
Sylivester Shumbusho Fundi kutoka Wakala wa Taifa wa Utafiti wa Nyumba
na Vifaa vya Ujenzi NHBRA akimpa maelezo Balozi Ombeni Sefue juu ya
utengenezaji wa matofali ya bei rahisi kwa kutumia udongo wakati
alipokuwa akitembelea karakana ya taasisi hiyo iliyopo Mwenge jijini Dar
es salaamKatikati ni Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Bw. Matiko Samson
Mturi.
Mkurugenzi
wa Taasisi hiyo Bw. Matiko Samson Mturi akimpa maelezo Balozi Ombeni
Sefue wakati alipokuwa akitembelea na kukagua shughuli mbalimbali katika
taasisi hiyo kulia ni Bw. Sylvester Shumbusho Fundi katika taasisi
hiyo.
Baadhi ya wafanyakazi wakiendelea na shughuli za kutengeneza vigae vya kuezekea nyumba katika karakana ya taasisi hiyo.
Balozi
Ombeni Sefue akitembezwa na Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Bw. Matiku
Samson Mturi maeneo mbalimbali ili kujionea shughuli za zinazofanywa
na taasisi hiyo.
Balozi
Ombeni Sefua akishiriki katika shughuli ya kufyatua matofali kazi
inayofanywa pia na Taasisi hiyo kwa kutoa mafunzo kwa vikundi mbalimbali
vya ujasiriamali nchini kote.
Balozi
Ombeni Sefua akiangalia kazi ya kufyatua matofali inayofanywa pia na
Taasisi hiyo kwa kutoa mafunzo kwa vikundi mbalimbali vya ujasiriamali
nchini kote.
Balozi Ombeni Sefue akiangalia wafanyakazi wa taasisi hiyo wakati wakitengeneza vigae kwa ajili ya kuezekea nyumba.
Balozi
Ombeni Sefue akipiga picha kwa simu yake huku wafanyakazi wa taasisi
hiyo wakimuangalia baada ya moja ya nyumba ndogo iliyojengwa katika
ghala ya taasisi hiyo kwa ajili ya mfano kumfurahisha.
Balozi
Ombeni Sefue pamoja na Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Bw. Matiko Samson
Mturi wakipiga picha ya pamoja na wafanyakazi wa taasisi hiyo mara baada
ya kukamilika kwa ziara hiyo.
No comments:
Post a Comment