Afya : Katibu Mkuu wizara ya Afya atemnelea makazi ya Wazee ya Kibirizi, Kigoma - Wazalendo 25 Blog

Breaking

Glory to Story.


Post Top Ad


30 Jul 2016

Afya : Katibu Mkuu wizara ya Afya atemnelea makazi ya Wazee ya Kibirizi, Kigoma


Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Generali Mstaafu Emmanuel Maganga mara baada ya kuwasili Mkoani hapo kwa ajili ya ziara ya kikazi ya kutembelea Makazi ya Wazee na watu wenye ulemavu ya Kibirizi.

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Generali Mstaafu Emmanuel Maganga akimueleza jambo Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga mara baada ya kuwasili Mkoani hapo kwa ajili ya ziara ya kikazi ya kutembelea Makazi ya Wazee na watu wenye ulemavu ya Kibirizi, Katikati ni Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa wa Kigoma Bw. Moses Msuluzya.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili Makazi ya Wazee na watu wenye ulemavu ya Kibirizi yaliyopo Mkoani Kigoma kwa ajili ya ziara ya kikazi.

Afisa Mfawishi wa Makazi ya Wazee na watu wenye ulemavu ya Kibirizi yaliyopo Mkoani Kigoma Bw. Ladius Mushi akimpa maelezo Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga kuhusu Makazi hayo na namna wanavyoshirikiana na wadau mbalimbali katika kuhakikisha Wazee hao wanakuwa katika mazingira salama.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga akiongozwa na wafanyakazi wa Makazi ya Wazee na watu wenye ulemavu ya Kibirizi yaliyopo Mkoani Kigoma kukagua baadhi ya majengo wanayoishi wazee hao ili kuona namna ya kuyaboresha kadiri inavyowezekana wakati wa ziara ya kikazi ya kutembelea Makazi hayo.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga akiongea na wafanyakazi wa Makazi ya Wazee na watu wenye ulemavu ya Kibirizi yaliyopo Mkoani Kigoma.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga akitoa Zawadi ya Sabuni kwa viongozi wa wazee wa Makazi ya Kibirizi Katibu Makazi hayo Bi. Veronica Nyaga na Mwenyekiti Bw.Hamisi Sabuni. Picha na Hassan Silayo-MAELEZO

Post Top Ad