Mchezo wa kwanza wa makundi Kombe la Shirikisho kati ya Bajaia ya Argeria
na Yanga, umemalizika hivi punde huko jijini Bajaia, huku Yanga wakikubari
kipigo cha bao1-0 dhidi ya Bajaia. Bao hilo lilifungwa na Yassin Salhi
katika dakika ya 20 na dakika ya 90+ beki wa kushoto wa Yanga Mwinyi Hajji,
alizawadiwa kadi nyekundu baada ya kumchezea faulo mshambuliaji wa Mo
Bajaia. Baada ya mchezo huo Yanga wanarejea nchini Uturuki kuendelea na
Kambi yao kwa ajili mchezo dhidi yao ya TP Mazembe unaotarajia kupigwa Juni
28 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam
NIT YASHEREHEKEA MIAKA 50 KWA UZINDUZI WA KITUO KIKUBWA CHA UMAHIRI
-
CHUO cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) kimeadhimisha miaka 50 tangu
kuanzishwa kwake kwa kuzindua Kituo Kikubwa cha Umahiri cha Usafiri wa Anga
na...
2 hours ago
No comments:
Post a Comment