Usalama barabarani : PUMA Energy yatangaza washindi wa shindano la kampeni ya usalama barabarani kwa shule za msingi Dar. - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Monday, 2 May 2016

Usalama barabarani : PUMA Energy yatangaza washindi wa shindano la kampeni ya usalama barabarani kwa shule za msingi Dar.


KAMPUNI ya Puma Energy Tanzania yawakabidhi zawadi washindi wa shindano la kampeni ya Usalama barabarani lililoshindanisha shule sita za jijini Dar es Salaam ambazo ni Maweni, Kimara Baruti, Oysterbay, Gongolamboto Jeshini na Mji Mwema.

Ndoto kubwa ya kampuni ya Puma Energy Tanzania  katika kuhakikisha usalama wa wanafunzi wakati wa kuvuka barabara ni kushirikisha shule zote za msingi Tanzania ili kuhakikisha watoto wako salama na ajali za barabarani.

 hayo yamesemwa na Meneja Mkuu wa Kampuni ya Mafuta ya Puma Energy Tanzania, Philippe Corsalrtti  wakati akizungumza na wanafunzi wa shule za Msingi sita za jijini Dar es Salaam katika wa hafla fupi ya kutafuta mshindi na kumtangaza kutokana na mchoro alioutoa kama unahamasisha uasalama barabarani, katika shindano hilo shule ya Gongolamboto Jeshini iliibuka mshindi baada ya kushinda wanafunzi wawili wa mchoro bora zaidi ya wengine na shule ya msingi Oysterbay kuwa na mshindi mmoja.

Nae Kamishina Msaidizi wa Polisi(ACP), Fortunatus Musilimu 
 amewaasa madereva watakiwa kufuata sheria za usalama barabarani ili kuepusha ajali na madhara yanayojitokeza barabarani hasa wakiona wanafunzi wanavuka barabara, ikiwa takwimu za mwaka 2015 zinaonyesha kuwa wanafunzi  78 walipoteza  na majeruhi  191 katika matukio tofauti hapa nchini 

 Maeneo hatari sana kwa wanafunzi kwa jijini la Dar es Salaam  amesema kuwa ni Lumumba, Mikumi, Mtambani, Boko-Basihaya Bunju na Kongowe.






Meneja Mkuu wa Kampuni ya Mafuta ya Puma Energy Tanzania, Philippe Corsalrtti akizungumza katika hafla ya kuwatangaza washindi wa kampeni ya Uasalama barabarani kwa wanafunzi wa shule za msingi zilizopo jijini Dar es Salaam. Shindano hilo lililoshirikisha shule sita za jijini Dar es Salaam kama, Shule ya Msingi Maweni, Kimara Baruti, Oysterbay, Gongolamboto Jeshini na Mji Mwema. Katika shindano hilo shule ya Msingi Gongolamboto Jeshini iliyopo manispaa ya Ilala iliibuka mshindi kwa kuwa na wanafunzi wawili kwa kufanikiwa kuchora mchoro unaoweza kutoa tahadhari katika usalama barabarani.
 Mkurugenzi wa Afrika wa kampuni ya AMENDI, Tom Bishop akizungumza katika hafla ya kuwakabidhi washindi wa shindano la kampeni ya usalama barabarani lililoandaliwa na kampuni ya Puma Enegy Tanzania jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Kamishina Msaidizi wa Polisi(ACP), Fortunatus Musilimu akizungumza na wanafunzi wa shule sita za jijini Dar es Salaam katika kutangaza mshindi wa shindano la Kapeni ya Usalama barabaranu kwa shule za msingi na kutangaza mshindi wa shindano hilo lililofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
 Kauli mbiu ya kuwalinda watoto na ajali za barabarani ambayo ni "Kwa pamoja hatutaki ajali tunataka kuishi na maendeleo" alisema Kamishina Msaidizi wa Polisi(ACP) huyo.
Baadhi ya wanafunzi wa shule za msingi za jijini Dar es Salaam wakiwa katika hafla ya kuwatafuta washindi wa shindano la kampeni ya usalama barabarani kwa shule za msingi iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Meza kuu wakiwa katika hafla ya kuwatafuta na kuwakabidhi washindi wa shindano la kampeni ya Usalama barabarani kwa shule za msingi sita za jijini Dra es Salaam.
 Mwalimu akiwaelezea wanafunzi wake igizo la jinsi ya kuepukana na ajali za barabarani.
 Mshehereshaji akiwasaidia wanafunzi kuimba wimbo wa kuhamasisha usalama barabarani wakati wanafunzi wanavuka barabara.
Meneja Mkuu wa Kampuni ya Mafuta ya Puma Energy Tanzania, Philippe Corsalrtti na Kamishina Msaidizi wa Polisi(ACP), Fortunatus Musilimu wakiangalia picha  kwaajili ya kupata picha inayoonyesha ujumbe wa kampeni ya usalama barabarani kwa shule za msingi sita za jijini Dar es Salaam. 
 Kamishina Msaidizi wa Polisi(ACP), Fortunatus Musilimu akionyesha picha ya mshindi wa tatu katika shindano la Kampeni ya Usalama Barabarani kwa shule za msingi shindano lililodhaminiwa na kampuni ya Puma Energy Tanzania. Mshindi wa Tatu ni Shaib Abdala darasa la 5 wa shule ya msingi, Gongolamboto Jeshini. kushoto aliyeshika begi ni Meneja Mkuu wa Kampuni ya Mafuta ya Puma Energy Tanzania, Philippe Corsalrtti.

 Kamishina Msaidizi wa Polisi(ACP), Fortunatus Musilimu akionyesha picha ya mshindi wa pili katika shindano la kuchora mchoro unaotoa taarifa ya usalama barabarani, Abdala Husein wa shule ya msingi Oysterbay jijini Dar es Salaam.
 Mshindi wa Kwanza wa shindano la Kampeni ya usalama Barabarani kwa shule za Msingi, Christina Christopher Darasa la Saba Shule ya Msingi, Gongolamboto Jeshini akisaidiwa  kutembea mara baada ya kutangazwa ndiye aliyechora mchoro mzuri zaidi ya wengine na kutangazwa kuwa mshindi wa shindano hilo na kupata mfano wa hundi ya shilingi milioni mbili kwaajili ya vitabu vya shule anayesoma.
 Kamishina Msaidizi wa Polisi(ACP), Fortunatus Musilimu  akionyesha mchoro wa Mwanafunzi Christina Christopher wa Darasa la saba shule ya Msingi Gongolamboto Jeshini (aliyeshika kikombe) mara baada ya kuibuka mshindi katika shindano lililoandaliwa na kampuni ya mafuta ya Puma Energy Tanzania lililofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
 Meneja Mkuu wa Kampuni ya Mafuta ya Puma Energy Tanzania, Philippe Corsalrtti akimkabidhi mwalimu wa shule ya Msingi ya ongolamboto Jeshini, Hashim Kalya akipokea mfano wa hundi ya shilingi milioni mbili mara baada ya  wanafunzi wa Darasa la saba wa shule hiyo Christina Christopher Kushoto mbele aliyeshika kombe ambaye ni mshindi wa kwanza wa shindano la Usalama barabarani kwa shule za Msingi.
Meneja Mkuu wa Kampuni ya Mafuta ya Puma Energy Tanzania, Philippe Corsalrtti na  Kamishina Msaidizi wa Polisi(ACP), Fortunatus Musilimu wakiwa katika picha ya pamoja na wawakilishi wa manispaa ya Ilala na Kinondoni pamoja na wanafunzi walioshinda katika shindano la usaama barabarani kwa shule za msingi za jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment