Picha ya Pamoja ya Majenerali na wakuu wa Majeshi ya nchi kavu Barani Afrika, Jijini Arusha
Picha ya Pamoja ya Majenerali na wakuu wa Majeshi ya nchi kavu Barani Afrika, Jijini Arusha
Picha ya Pamoja ya Majenerali na wakuu wa Majeshi ya nchi kavu Barani Afrika, Jijini Arusha
Na Ferdinand Shayo wa Wazalendo 25 Blog ,Arusha.
Majenerali
na Wakuu wa Majeshi ya nchi kavu Barani Afrika wamekutana jijini Arusha
kujadili changamoto zinazoyakibili majeshi hayo ikiwemo tishio la ugaidi
,biashara ya madawa ya kulevya suala linalopelekea majeshi hayo kuunganisha
nguvu katika kupambana na matukio hayo.
Mnadhimu
Mkuu wa Jeshi Luteni Jenerali Venance Mabeyo amesema kuwa majeshi ya nchi za
Afrika kwa kushirikiana na jeshi la Marekani lenye teknolijia kubwa iwapo
watashirikiana na Majeshi ya Afrika
kupambana na tatizo la ugaidi na kufanikiwa
Katibu Mkuu
wa Wizara Ulinzi na Majeshi Job amesema kuwa jeshi la Tanzania limejipanga
kukabiliana na vitendo vya ugaidi ambavyo kwa nchi ya Tanzania jukumu hilo
linafanywa na jeshi la polisi kwa kushirikiana na vyombo vingine.
Mnadhimu
wa Jeshi Marekani Jenerali Mark Milley pamoja na Balozi wa Marekani nchini Mark
Childress wamesema kuwa Marekani inasubiri kupata mawazo mapya kutoka kwa majeshi
ya Afrika juu ya namna ya kuimarisha uwezo na nguvu za kukabiliana na
changamoto za kiusalama.
Wakuu wa
Majeshi ya nchi Kavu wamekutana jijini Arusha kujadili juu ya changamoto
zinazoyakabili majeshi hayo ,na kubadilishana uwezo ili kuwawezesha kupiga hatua katika mapambano dhidi ya
ugaidi,madawa ya kulevya,usafirishaji wa binadamu pamoja na uhalifu.
No comments:
Post a Comment