Mbunge wa Karatu Wile Qambalo.
Mwenyekiti wa Baraza la Madiwani Halmashauri ya Karatu Jubilate Mnyenye.
Mkuu wa Wilaya ya Karatu Omary Kaang.
NA VERO IGNATUS wa Wazalendo 25 Blog - KARATU
Baraza
la Madiwani katika Halmashauri ya Karatu limewasimamisha kazi baadhi ya
watumishi kutokana na ubadhilifu wa fedha za Umma.
Mwenyekiti
wa Baraza la madiwani wa Halmashauri ya Karatu Jubilate Mnyenye
amewataja waiosimamishwa ni Dr.Thobias Nkina ambaye alikuwa mganga
mkuu,Judas Mahuma -Afisa Ardhi, George Ndimbo aliyekuwa Mhasibu,Jonathan
Rukuntuka-Mtunza fedha,Sigfred Njanga-Mtunza fedha,Rajabu Lingoni
alikuwa Muweka Hazina na Gurisha Kavuga -Mtunza stoo, wote hawa
wamesimamishwa kwaajili ya uchunguzi.
Amesema
kuwa kutokana na tume ya uchunguzi iliyoundwa mwezi mmoja uliopita na
kamati ya fedha ya Halmashauri ,ikitaka kufahamu mapato na matumizi ya
Kilimo na Afya ,ilibaini mambo kadhaa ambayo iliwasilisha kwenye.kikao
kwaajili ya maamuzi,ndipo kamati ya madiwani ilipoamua kuchukua hatua ya
kuwasimamisha .
Sambamba
na hayo wapo watumishi ambao wamepewa onyo ambao ni Afisa Elimu Bernad
Mnyenyelwa, Dr.Kyabaroti Kyabaroti pamoja na Omari Shemdiru,ambapo wapo
watumishi wengine 8 ambao wanapaswa kurudisha fedha walizozichukua
shilingi milioni 81 kama masurugu ya kufanyia shughuli mbalimbali za
idara zao ndani ya siku 14.
Kwa
maelezo ya baraza la madiwani limeomba wizara inayohusika kwa
mkutugenzi huyo imuwajibishwe kwa kuisababishia Halmashauri hasara ya
milioni 800 na kushindwa kuwasimamia watumishi wake na huku miradi ya
kilimo na Afya ikiathirika.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Karatu Moses Mabula.
Naye
Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Moses Mabula amesema kuwa alipohamia
katika.Halmashauri ya Karatu mwaka 2013 alikuta zimetumi zaidi ya
milioni 200 pia ameongeza kuwa Halmashauri iliazima fedha kwaajili
yakutekeleza miradi ya dharura,kati ya miradi hiyo ni pamoja na
ukarabati wa stendi kuu ya Karatu,Zahanati ya Ayalabe iliyoungua
moto,Ujenzi wa.madarasa 4 katika.shule ya msingi Ayalabe ili kupisha
chuo ,ukamilishaji wa mitaro katika jengo la.halmashauri,ujenzi wa
mahabara Endara na Mang'ola,Ujenzi wa madarasa katika shule ya msingi
Manusway,Ukamilishaji wa hostel ya wasichana katika shule ya sekondari
Kansay .
Hata
hivyo Moses Mabula amesema kuwa fedha zote ziliripotiwa katika baraza
lililopita la madiwani 2015,pia amesema.ameyapokea.malalamiko yote na
atawajibu baraza namna fedha zilivyotumika.
No comments:
Post a Comment