Taswira: Meya wa Jiji la Arusha Afanya Ziara Soko la Kilombero na Kukagua Maboresho ya Miundombinu ya Soko na eneo la Stendi ya muda - Wazalendo 25 Blog

Breaking

Glory to Story.


Post Top Ad


2 May 2016

Taswira: Meya wa Jiji la Arusha Afanya Ziara Soko la Kilombero na Kukagua Maboresho ya Miundombinu ya Soko na eneo la Stendi ya muda
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Jiji la Arusha Mh Kalisti Lazaro (mwenye suti) akizungumza na wafanyabiashara nje ya soko la Kilombero lililoko Kata ya Levolosi Jijini akiwa kwenye ziara ya kukagua maboresho ya miundo mbinu ya soko hilo na stand ya ya muda ya daladala nje ya eneo la soko leo.

Katika ziara hiyo Mh Meya Kalisti alimbatana na Diwani wa Kata ya Levolosi pamoja na Menej wa Soko la Kilombero.

Mstahiki Meya ameeleza kuridhishwa na maendeleo ya uboreshaji miundombinu na kuwahimiza wafanyabiashara kupaza sauti  zao ili Halmashauri iweze kufahamu kwa upande wao wanahitaji nini zaidi kiboreshwe sambamba na mfumo bora wa uendeshaji soko hilo.
Mstahiki Meya (kushoto) akiwasili eneo la stand ya muda ya daladala jirani na soko la Kilombero ambapo zoezi la kusambaza kifusi kufuatia uharibufu wa mvua likiwa linaendelea. Kushoto kwake ni mfanyabiashara Bw Yegella na Diwani wa Levelosi Mh Nanyaro (mwenye sweta)Diwani wa Levolosi Mh Ephata Nanyaro akikagua zoezi la umwagaji kifusi kwa ajili ya maboresho katika eneo la stand ya muda ya daladala Kilombero Jijini Arusha., siku ya Aprili 26, 2016

Post Top Ad