Mwenyekiti wa Mtaa wa Ilikiurei Kata ya Kiranyi Jimbo la Arumeru Magharibi Mh Onesphoy Chami (mwenye beleshi) pamoja Mwenyekiti wa Mtaa jirani wa Namayana Mh Elias Naigisa wote kupitia CHADEMA wakishiriki kwa pamoja na wananchi wa mitaa hiyo kuweka kifusi katika maeneo korofi ya barabara ya "Kwa Trafiki" kuelekea shule ya Ilikiurei yenye urefu wa tarkivani kilometa 2.5.
Ukarabati huu ni jitihada binafsi za viongozi hao katika kukabilina ana kero mbalimbali katika mitaa wanayoiongoza huku wakiwa na nguvu kazi kubwa nyuma yao.
Wananchi wa Ilikurei na Namayana wakishiriki ukarabati wa barabara yao
Wenyeviti wa Miataa ya Ilikurei na Namayana Kata ya Kirani ArumeruMagharibi wakishiriki kuhimiza wananchi kujitolea kukarababti njia za mitaa
Gari ikimwaga kifusi
Mwenyekiti wa Mtaa wa Ilikurei akishiriki kupanga mawe barabarabi kabla ya kumwaga kifusi ili kuziwezesha njia za mtaa kupitika kipindi hiki cha mvua.
No comments:
Post a Comment