Matukio : Uzinduzi wa mpango mpya wa kugawa vyandarua vyenye viuwatilifu kwa wakina mama wajawazito na watoto wafanyika mkoani Mtwara - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633


PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0676 643 633

Monday, 30 May 2016

Matukio : Uzinduzi wa mpango mpya wa kugawa vyandarua vyenye viuwatilifu kwa wakina mama wajawazito na watoto wafanyika mkoani Mtwara


Baadhi ya watoto wa mkoani mtwara wakishindana kucheza muziki ikiwa ni sehemu ya burudani zilizosindikiza hafla ya uzinduzi wa mpango wa kugawa bure vyandarua vyenye viuwatilifu kwa wakina mama wajawazito na watoto wenye umri wa chini ya miezi tisa ujulikanao kama kliniki chandarua.
Wasanii Joe makini na Niki wa pili kutoka kundi la weusi wakitumbuiza hadhara iliyojitokeza katika uzinduzi wa mpango wa kugawa bure vyandarua vyenye viuwatilifu kwa wakina mama wajawazito na watoto wenye umri wa chini ya miezi tisa ujulikanao kama kliniki chandarua 
Msanii wa nyimbo za taarab isha mashauzi akiimba moja ya kibao chake wakati akitoa burudani kwa wakazi wa mkoa wa mtwara waliohudhuria hafla uzinduzi wa mpango mpya wa kugawa vyandarua vyenye viuwatilifu kwa wakina mama wajawazito na watoto wenye umri chini ya miezi tisa ujulikanao kama kliniki chandarua
Msanii wa nyimbo za taarab isha mashauzi akitoa burudani kwa wakazi wa mkoa wa mtwara waliohudhuria uzinduzi wa mpango mpya wa kugawa vyandarua vyenye viuwatilifu kwa wakina mama wajawazito na watoto wenye umri chini ya miezi tisa ujulikanao kama kliniki chandarua
Mkuu wa mkoa wa mtwara halima dendego akimbeba mmoja ya watoto waliokabidhiwa chandarua chenye viuwatilifu ikiwa ni sehemu ya hafla ya uzinduzi wa mpango mpya wa kugawa vyandarua vyenye viuwatilifu kwa wakina mama wajawazito na watoto wenye umri chini ya miezi tisa ujulikanao kama kliniki chandarua
Mkuu wa mkoa wa Mtwara Halima Dendego akirusha maputo angani kuashiria uzinduzi wa mpango mpya wa kugawa vyandarua vyenye viuwatilifu kwa wakina mama wajawazito na watoto wenye umri chini ya miezi tisa ujulikanao kama kliniki chandarua
Mkuu wa mkoa wa Mtwara Halima Dendego akimkabidhi chandarua chenye viuwatilifu mmoja ya mama wajamzito ikiwa ni sehemu ya hafla ya uzinduzi wa mpango mpya wa kugawa vyandarua vyenye viuwatilifu kwa wakina mama wajawazito na watoto wenye umri chini ya miezi tisa ujulikanao kama kliniki chandarua
Mkuu wa mkoa wa Mtwara Halima Dendego akimkabidhi chandarua chenye viuwatilifu mmoja ya mama wenye watoto wa chini ya umri wa miezi sita ikiwa ni sehemu ya hafla ya uzinduzi wa mpango mpya wa kugawa vyandarua vyenye viuwatilifu kwa wakina mama wajawazito na watoto wenye umri chini ya miezi tisa ujulikanao kama kliniki chandarua

Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa mapambano dhidi ya Malaria wameendelea na jitihada za kupambana na ugonjwa huo ili kufikia lengo la serikali la kupunguza vifo hadi kufikia asilimia moja ifikapo mwaka 2020.

Katika kutekeleza azma hiyo, serikali ya Tanzania na wadau hao wamezindua mpango wa kugawa vyandarua vyenye viuwatilifu vya muda mrefu kwa akina wajawazito na watoto wenye umri wa chini ya miezi tisa.

Akizindua mradi huo kitaifa, mkuu wa mkoa wa Mtwara Bi Halima Dendego amewataka wanawake kuhudhuria kliniki wakati wa ujauzito ili kupata ushauri na kinga dhidi ya malaria ikiwa ni pamoja na kupata chandaru kitakacho mkinga dhidi ya ugonjwa huo.Amesisitiza suala la kusafisha ameneo yote ili kudhibiti mazalia ya mbu waenezao Malaria ikiwa ni njia moja wapo ya kupambana na kuenea kwa ugonjwa huo unaosababisha vifo vya wakina mama wajawazito na watoto wa chini ya miaka 5.

“kwa mujibu wa Takwimu za ugonjwa huo kwa mkoa wa Mtwara, zimeshuka kutoka asilimia 33 mwaka 2007/2008 hadi kufikia asilimia 17 kwa mwaka 2011/2012. Hata hivyo takwimu za kitaifa zinaonesha kushuka kwa ugonjwa huo kutoka asilimia 33 mwaka 2007/2008 hadi kufikia asilimia 9 mwaka 2015”. Alisema Bi Dendego.“Lengo la kitaifa la mapambano dhidi ya Malaria linaonesha kupunguza vifo hivyo hadi kufikia asilimia 5 mwaka huu na asilimia 1 mwaka 2020 hivyo sisi mkoa wa Mtwara tuna jukumu la kuhakikisha takwimu zetu zinaenda sambamba na takwimu za kitaifa”. Amesisitiza Mkuu huyo wa mkoa.

Kwa upande wake Naibu Mkurugenzi wa kutoka ofisi ya Afya ya shirika la misaada la Marekani USAID Bibi Ana Bodipo -Memba amesema, ushirikiano wa serikila ya Marekani na Tanzania katika mapambano dhidi ya Malaria umeonesha mafanikio makubwa kwani wamefanikiwa kupunguza kwa silimia 50 vifo vitokanavyo na malaria kwa upande wa Tanzania Bara na chini ya asilimia moja kwa upande wa Zanzibar.

“Marekani inafahamu umuhimu wa mapambano dhidi ya Malaria, na hivyo mfuko wa Rais wa Kupambana na Malaria kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kupunguza vifo hivyo nah ii ni ishara nzuri katika kufikia malengo ya kuutokomeza kabisa ugonjwa huu.” Alisema Bi Bodipo.

Mwakilishi wa wizara ya Afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto Bi Helen Semu amesema, serikali itaendelea na uhamasishaji wa jamii kuendelea kutumia vyandarua vyenye viuwatilifu ili asilimia 85 iliyofikiwa kwa sasa izidi kuongezeka na kufikia lengo la kumaliza kabisa tatizo hilo nchini.“Sisi Serikalini tutahakikisha tunaongeza jitihada za kuhamasisha jamii kuendelea kutumia vyandarua vyenye viuwatilifu ili kila mmoja afahamu umuhimu wa kufanya hivyo na kudhibiti maambukizi na vifo vitokanavyo na ugonjwa huu” alisema bi Helen

Mpango wa utoaji vyandarua vyenye viuwatilifu kwa akina mama wajawazito na watoto wenye umri wa chini ya miezi tisa ujulikanao kama CHANDARUA KLINIKI unachukua nafasi ya mpango wa zamani wa HATIPUNGUZO na unasimamiwa na Mradi wa VECTORWORK kwa kushirikiana na serikali ya Tanzania na unfadhiliwa na mfuko wa Rais wa Marekani wa kupambana na Malaria chini ya usimamizi wa shirika la misaada la nchi hiyo – USAID.

No comments:

Post a Comment