Mkuu
wa chuo cha Kodi (TRA), Profesa Isaya Jairo akizungumza wakati wa
hafla kufungua mafunzo ya awamu yapili ya wafanyakazi wa mamlaka ya
mapato Tanzania(TRA) Amesema kuwa wameamua
kuanzisha mpango huo kwa kushirikiana na Mamlaka ya mapato ili
kufundisha wafanyakazi wa TRA maadili na nyenzo za utendaji
kazini pamoja na kuendesha mafunzo ya dini ili kuwafanya wafanyakazi
wawe wacha Mungu katika kazi zao.
Kaimu
Mkurugenzi Rasilimali Watu na Utawala wa TRA, Victor Kimaro akizungumza
na wafanyakazi wa malaka ya Mapato Tanzania(TRA) wakati wa kufungua
mafunzo ya awamu ya pili kwa wafanyakazi wake 200. Pia amewataka
wafanyakazi wote wanatakiwa wafanye kazi kwa maadili hususani upande wa
ukusanyaji kodi na Chuo hicho kimewafundisha wafanyakazi hao kufanya
kazi kwa ushindani katika maeneo ya kazi ili kuliletea taifa maendeleo
yaliyokusudiwa.
Kamishna
Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Alphayo Kidata akizungumza na
wafanyakazi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) jijini Dar es Salaam
leo. wakati wa kufungua mafunzo ya maadili kwa wafanyakazi wa TRA ambao
wamefanya usaili na kufanikiwa kufunzu kusoma mafunzo hayo kwa
wafanyakazi kwaajili ya kujifunza mambo mtambuka ya tasinia ya TRA.
Lengo la kuwapa mafunzo hayo ni kutaka kuijenga Mamlaka ya Mapato (TRA)
mpya.Kulia ni Mkuu wa chuo cha Kodi (TRA), Isaya Jairo na Kushoto ni
Kaimu Mkurugenzi wa Rasiliamali watu na utawala katika chuo cha
Kodi(TRA), Victor Kimaro wakiwa katika mkutano wa kufungua mafunzo ya
wafanyakazi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA).
Kamishna
Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Alphayo Kidata akizungumza na
wafanyakazi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA)leo jijini Dar es Salaam.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Alphayo Kidata na Mkuu wa chuo cha Kodi (TRA), Profesa Isaya Jairo wakikata utepe kuzindua ripoti ya mafunzo kwa wanafunzi wa malaka ya Mapato Tanzania jijini Dar es Salaam leo.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Alphayo Kidata (Katikati walioshika vitabu ),Mkuu wa chuo cha Kodi (TRA), Profesa Isaya Jairo(Kulia) na Kaimu
Mkurugenzi Rasilimali Watu na Utawala wa TRA, Victor Kimaro (kushoto)
wakionyesha vitabu vya mafunzo kwa wafanyakazi wa TRA jijini Dar es
Salaam leo.
Kamishna
Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Alphayo Kidata akiwa katika
picha ya pamoja na wafanyakazi wa TRA jijini Dar es Salaam leo.
Wafanyakazi hao ndio wanaohudhulia mafunzo hayo.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Alphayo Kidata amesema kuwa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) imebakiza Tsh. Trilioni 2.363 ili kufikia lengo walilojiwekea la kukusanya mapato ya trilioni 12.363 katika mwaka wa fedha 2015/16, ambapo hadi sasa imekusanya kiasi cha Tsh. Trilioni 10. Ameyasema hayo wakati wa hafla ya uzinduzi wa awamu ya pili ya mpango wa mafunzo kwa wafanyakazi waliopo kwenye fursa ya ajira za taasisi hiyo.
Mkuu wa chuo cha Kodi (TRA), Profesa Isaya Jairo.
No comments:
Post a Comment