MFANYAKAZI
wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Nchini, TAA, akiielekeza ndege ya
Shirika la Ndege Mauritius Airlines, kuegesha kwenye daraja la kushukia
abiria (Bridge), kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere
jijini Dar es Salaam, Mei 6, 2016. Ndege hiyo aina ya Airbus 319 yenye
uwezo wa kubeba abiria 130, imetua kwa mara ya kwanza na itakuwa
ikifanya safari zake kila Ijumaa ikiruka moja kwa moja kutoka Mauritius
kuja Dar es Salaam kasha Nairobi, nchini Kenya.
Magari ya zimamoto yakiipokea ndege hiyo kwa kuimwagia maji ikiwa ni ishara ya ukaribisho
NA K-VIS MEDIA/Khalfan Said, JNIA
Mamlaka
ya Viwanja vya Ndege Nchini, TAA, kupitia uwanja wake wa ndege wa
Kimataifa wa Julius Nyerere, imeongeza idadi ya mashirika ya ndege
yanayotumia uwanja huo baada ya ndege ya kwanza ya Shirika la Ndege la
Mauritius (Mauritus Airlines), kutua kwenye uwanja huo Mei 6, 2016.
Ndege
hiyo aina ya Boeng Airbus 319, yenye kubeba abiria 130, ilitua kwenye
uwanja huo majira ya saa 5;20 asubuhi ambapo kama ilivyoada ya kupokea
ndege mpya inayoanza shughuli zake kwenye uwanja huo, magari mawili ya
zimamoto yalipiga (saluti), kumwagilia maji ndege hiyo wakati ikielekea
kuegesha kwenye daraja la kushukia abiria.
Kwa
mujibu wa maafisa wa Shirika hilo, ndege hiyo itakuwa ikiruka kutoka
Mauritius moja kwa moja na kutua kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa
Julius Nyerere ambapo itashusha abiria na kuelekea uwanja wa ndege wa
Jomo Kenyatta.
“Safari ya kutoka Mauritius kuja Dar es Slaam ni kiasi ya masaa matatu .”alisema rubani mkuu wa ndege hiyo, Parikshant Nundlol
Maafisa wa TAA waliiambia K-VIS MEDIA kuwa ndege hiyo itakuwa ikifanya safari yake mara moja kwa wiki kila siku ya Ijumaa.
Rubani mkuu wa ndege hiyo, Parikshany Nundlol, akizungumza na waandishi wa habari wa Mauritius waliofuatana na ndege hiyo.
Warembo wa Kitanzania walioshiriki kuipokea ndege hiyo.
Wafanyaakzi wa shirika la ndege la Mauritius na wale wa Swissport wakiwa katika picha ya pamoja.
Abiria wa kwanza waliowasili na ndege hiyo.
No comments:
Post a Comment