Tarehe 23
April, 2016.... ilitimia miaka 400 tangu gwiji wa fasihi, mashairi na
tamthiliya, mwandishi maarufu wa Kiingereza, William Shakespeare alipofariki. Mwasisi wa taifa la Tanzania ,Mwalimu
Julius Nyerere aliwahi kutafsiri Kiswahili
kazi mbili za Shakespeare :” Mabepari wa Venice” (Merchants of Venice)
na “ Julius Kaizari” (Julius Caesar) ...
Wasanii mbalimbali duniani wamekuwa wakijumuika kutukuza kazi za nguli huyu asiyechuja kwa visa, lugha, nahau, misemo na mada za kila namna. Miongoni mwao ni kundi maalum - “Bards without Borders” (Watenzi Wasio na Mipaka), jijini London. Ndani wamo washairi wa Somalia, Nigeria, Bangladesh, Zimbabwe, Jordan, Colombia, Afghanistan, Bosnia, Ujerumani, Jamaica, Uingereza, India na Tanzania. Mwakilishi wa Tanzania ni mwandishi Freddy Macha. Anatumia muziki wa ala mbalimbali ikiwemo Ngoma kumnadi Shakespeare.

Wakati maonesho mbalimbali yakiendelea kwa kasi
Uingereza, Macha ametafsiri kazi zake Shakespeare kwa Kiswahili na pia kuandika
tenzi mpya na kikundi hiki. Moja ya tukio lililofanyika April 23 , klabu mashuhuri ya Rich Mix, London mashariki,
Macha alichanganya mapigo ya Ngoma
kadhaa za Kiafrika ikiwepo Sindimba ya
Tanzania kutambika na kumsifia gwiji William Shakespeare.
VIDEO
HABARI ZAIDI
No comments:
Post a Comment