Elimu : SSRA yatoa elimu kwa umma kwa wakulima, vyuo vya ualimu na VETA katika mikoa ya Ruvuma , Njombe na Simiyu - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633


PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0676 643 633

Friday, 20 May 2016

Elimu : SSRA yatoa elimu kwa umma kwa wakulima, vyuo vya ualimu na VETA katika mikoa ya Ruvuma , Njombe na Simiyu


Waelimishaji kutoka Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi (SSRA), wakiwa katika picha ya pamoja na wadau wa Chuo cha Ualimu Matogoro, Songea, mkoani Ruvuma, wakati mamlaka hiyo, ilipokuwa ikitoa elimu kwa umma hivi karibuni.
Baadhi ya wakulima wa Mkoa wa Ruvuma wakifuatilia mada ya Hifadhi ya Jamii kutoka SSRA wakati wa semina za elimu kwa umma zilizoendeshwa na Mamlaka hiyo.
Mkuu Kitengo cha Ununuzi wa SSRA, Bw. Emmanuel Urembo, akitoa mada kwa wanafunzi wa Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) Mjini Songea.
Wakulima wa Mkoa wa Njombe, wakisikiliza mada kuhusu Hifadhi ya Jamii kutoka kwa waelimishaji wa SSRA, wakati wa semina za elimu kwa umma zilizoendeshwa na SSRA mkoani humo hivi karibuni.
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Uhamasishaji wa SSRA, Bi. Saraha Kibonde Msika, akitoa ufafanuzi kuhusu masuala mbalimbali ya Hifadhi ya Jamii kwa wanafunzi wa Chuo cha Ufundi Stadi (VETA), Makete hivi karibuni.
Waelimishaji kutoka SSRA, Bi. Sarah Kibonde Msika (katikati) na Bw. David Lyanga (kulia mbele), wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Chuo cha Ualimu Hagafilo Njombe.
Ofisa kutoka SSRA, Bw. David Lyanga akitoa mada kuhusu Hifadhi ya Jamii wakati wa semina za elimu kwa umma zilizoendeshwa na SSRA, mkoani Njombe hivi karibuni.
Waelimishaji kutoka SSRA, Bi. Sarah Kibonde Msika (katikati) na Bw David Lyanga (wa pili kushoto), wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi na wanafunzi wa Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) Makete, mkoani Njombe hivi karibuni.
Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa SSRA, Bw. Peter Mbelwa akitoa maelezo kuhusu masuala ya Hifadhi ya Jamii wakati wa Semina iliyoandaliwa na Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), iliyofanyika kwa Wanachuo  na Wafanyakazi wa Chuo cha Ufundi Binza, kilichopo Wilaya ya  Maswa, mkoani Simiyu hivi karibuni.
Ofisa uhusiano wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Bi. Agnes Lubuva akitoa mada ya Hifadhi ya Jamii kwa wanafunzi na wafanyakazi wa Chuo cha Ufundi Binza kilichopo Wilaya ya Maswa, mkoani Simiyu, hivi karibuni.
Wafanyakazi wa SSRA wakiwa katika picha ya pamoja na Wanachama wa Mtandao wa vikundi vya Wakulima (MVIWATA), baada ya kupata Semina ya Hifadhi ya Jamii iliyofanyika Bariadi, Kata ya Lugulu, hivi karibui. (Picha zote na SSRA)

No comments:

Post a Comment