Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya CRDB Dk. Charles Kimei leo tarehe 18/05/2016
amezungumza na waandishi wa habari jijini Arusha na kuzungumzia kuhusu
mkutano mkuu wa wanahisa wa Benki ya CRDB unaotarajia kufanyika jijini
Arusha tarehe 21/05/2016 katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa
AICC.
Mkutano
huo wa wanahisa wa Benki ya CRDB utatanguliwa na semina maalum kwa
wanahisa wa Benki hiyo itakayofanyika tarehe 20/05/2016 katika ukumbi
huo huo ambapo pamoja na mambo mengine wanahisa wa Benki ya CRDB
watapata kufahamu juu ya fursa mbalimbali zinazopatikana kwa kuwa sehemu
ya wanahisa wa Benki hiyo.
Dk.
Kimei amechukua fursa hiyo kuwakaribisha wanahisa wote wa Benki ya CRDB
kuweza kushiriki katika semina na mkutano mkuu na kusisitiza kuwa
mkutano wa mwaka huu utakua ni wa kipekee ikizingatiwa kuwa Benki ya
CRDB ipo katika maadhimisho ya miaka 20 tangu ilipoanza rasmi mnamo
mwaka 1996 baada ya utekelezaji wa sera ya ubinafsishaji nchini.
Mkurugenzi
Mtendaji wa
Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei (katikati) akionyesha kitabu cha
taarifa ya
Mwaka ya benki hiyo wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini
Arusha. Kushoto ni Naibu Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Huduma Shirikishi,
Esther
Kitoka na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Uendeshaji na Huduma kwa Wateja,
Saugata
Bandyopadhyay. Benki hiyo inatarajia kufanya mkutano mkuu wa wanahisa
Mei
21. (Na Mpigapicha Wetu)
Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akifafanua jambo wakati wa
mkutano na waandishi wa habari jijini Arusha.
Baadhi ya wafanyakazi wa
Benki ya CRDB wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles
Kimei (hayupo pichani) wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Arusha
jana. Kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja,
TullyEsther Mwambapa, Mameneja wa Idara hiyo Ena Mwangama na Godwin Semunyu.
No comments:
Post a Comment