Michezo : Vijana watakiwa kushiriki michezo ili kujiepusha na makundi maovu - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Thursday, 19 May 2016

demo-image

Michezo : Vijana watakiwa kushiriki michezo ili kujiepusha na makundi maovu



13230059_1233123720053909_39788261670440787_n
 Aliekuwa mgombea wenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha Emanuel Makongoro akiwa amnawapa mawaidha wachezaji kabla ya mechi kuanza
13226823_1233123386720609_4347999824396014876_n
  mwenyekiti wa CCM  kata ya Sakina Neema Molel ambaye pia ni mwaandaaji wa  tamasha la vijana akiwa anasalimiana na wachezaji wa moja ya timu ambazo zimeshiriki tamasha hilo


13230265_1233123336720614_6779840162753238115_n


13233064_1233122810054000_21269064126699127_n


13240726_1233122600054021_7498495936961327965_n
Aly Mtumwa katikati akiwa anabadilishana mawazo na Aliekuwa mgombea wenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha Emanuel Makongoro
13240750_1233123686720579_8587463651892238496_n
 Alikuwa mgombea ubunge wa viti maalumu wazazi kupitia tiketi ya chama cha mapinduzi  ,ambaye pia ni mkurugenizi wa Phideintatament Phidesia Mwakitalima akiwa anasalimiana na timu kabla ya mechi za siku hiyo kuanza
13254251_1233123196720628_3283395768134495458_n
 muandaaji wa mashindano hayo  wa kwanza kulia Neema molel akifuatana na mkufunzi ambaye ni mkurungezi wa kituo cha kukuza vipaji vya vijana (Rolling stone)Ally Mtumwa tayari kwa kukagua timu kabla ya mechi kuanza
13254365_1233122696720678_827872162246040724_n


13254612_1233123493387265_8543984458402597662_n
 naye muimbaji wa nyimbo za injili  Neema Kasambale nae pia aliudhuria kuangalia jinsi vijana wanavyo sakata kabumbu
13256446_1233123076720640_5193249866910850114_n


13267927_1233122753387339_7736707903033826800_n


13267927_1233123270053954_523536777453396960_n
 mwenyekiti wa CCM  kata ya Sakina Neema Molel ambaye pia ni mwaandaaji wa  tamasha la vijana akiwa anasalimiana na wachezaji wa moja ya timu ambazo zimeshiriki tamasha hilo
13254548_1233123016720646_7023351815041801278_n
 wachezaji wakiendelea kusakata kandanda ndani ya kiwanja cha ngarenaro mkoani arusha
13265941_1233122970053984_76271515759980729_n
mashabiki pia waliudhuria kuangalia baadhi ya mechi
Na Woinde  Shizza,Arusha
 vijana wametakiwa kujijengea tabia ya kushiriki michezo mbalimbali kila mara badala ya kujiingiza katika makundi mabaya ya wizi pamoja na utumiaji wa madawa ya kulevya kitu ambacho kinawaaribia mfumo mzima wa maisha yao.
 Hayo yamebainishwa na mwenyekiti wa CCM  kata ya Sakina Neema Molel ambaye pia ni mwandaaji wa Tamasha vijana la mpira wa miguuu linaloendeshwa kwa mfumo wa ligi ya mpira wa miguu linayowashirikisha vijana kutoka katika kata ya sakina . 
 Alisema kuwa yeye kama mama anaumia sana kuona vijana wanakaa mitaani na kujiingiza katika vitendo mbalimbali mbali ikiwemo wizi pamoja na utumiaji wa madawa ya kulevywa ivyo ameamua kuanzisha ligi hii ili kuwasaidia vijana wengi kushiriki na kuachana na makundi .
 "unajua pia michezo ni ajira hivyo nimeona ni vyema mimi kama mama kiongozi wa watoto nianzishe ligi hii ya mpira wa miguu ili awa vijana wetu waweze kushiriki,kujifunza na pia ule mda walikuwa wanatumia kwenda kuangaika uko mtaani na kutumia madawa ya kulevywa watakuja apa watashiriki michezo "alisema Neema
 Aidha alibainisha kuwa ligi hii aitaishia kipindi hichi kwani itakuwa endelevu na ameamua kuanza na watoto wa kiume kwa kuanzisha mpira wa miguu lakini pia anania yakuanzisha ligi ya wanawake ya mpira wa pete ili pia kuwawezesha watoto wakike nao kujitokeza na kujifunza kwani michezo pia ni ajara pamoja na afya. 
 Kwa upande wake Aliekuwa mgombea wenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha ambaye alikuwa mgeni rasmi katika siku hii ya uzinduzi wa mashindano hayo Emanuel Makongoro alisema kuwa amefurahishwa sana kuona jinsi vijana walivyojitokeza kushiriki ligi hiii kwani wametambua umuimu wa michezo katika afya zao. 
 Aliwasihi vijana kuachana nakujishulisha na biashara za madawa ya kulevya pamoja na unywaji wa pombe za makaratasi(viroba) badala yake washiriki katika michezo mbalimbali na hata kama amna ligi basi washiriki katika mazoezi kwani wakifanya mazoezi yanaweza kuwasaidia kuondokana na vishawishi mbalimbali vinavyoweza kuwapata .
 Kwa upande wa aliyekuwa mgombea ubunge viti maalumu wa wazazi CCM mkoa wa Arusha Phidesia Mwakitalima alisema kuwa timu hizo bado zinakabiliwa na changamoto nyingi hivyo wanaitaji wadhamini na wafadhili wakubwa kujitokeza ili kuweza kunyanyua vipaji vya vijana hao wa Kata ya sakina pamoja na Kata zote za mkoa wa Arusha 
Aidha alisema kuwa wakiwawajenga vijana katika michezo itasaidia kupunguza makundi mabaya mitaani na kupelekea vijana kujituma. Ligi hii ya Tamasha la vijana wa Sakina limeanza rasmi mapema mwanzoni mwa mwezi huu na inatarajiwa kumalizika jumapili ambapo mshindi atapatiwa zawadi mbalimbali ikiwemo makombe ,jezi pamoja na mipira .

No comments:

Post a Comment

Tuwasiliane

Name

Email *

Message *

Contact Form

Name

Email *

Message *