
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
(kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Daktari dhamana wa Kituo cha
Maradhi ya Kipindupindu Ramadhan Mikidadi Suleiman leo asubuhi
alipotembelea kituoni hapo Chumbuni karakana Wilaya ya Magharibi
Unguja,wengine ni Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo(wa pili kushoto)
na naibu Waziri wa Wizara hiyo Harusi Said Suleiman na Katibu Mkuu
Dkt.Juma Malik Akili (katikati).

Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
akipata maelezo kutoka Mkurugenzi kinga Wizara ya Afya Dk.Mohamed Dahoma
(katikati) wakati alipotembelea Kituo cha Maradhi ya Kipindupindu hapo
Chumbuni karakana Wilaya ya Magharibi Unguja leo asubuhi,wengine ni
Daktari dhamana wa Kituo cha Maradhi ya Kipindupindu Ramadhan Mikidadi
Suleiman (kushoto)Mkurugenzi Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt.Jama Adam
Taib(wa pili kushoto).

Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
akitoa maelezo kwa Uongozi wa Wizara ya Afya wakati alipotembelea Kituo
cha Maradhi ya Kipindupindu hapo Chumbuni karakana Wilaya ya Magharibi
Unguja leo asubuhi,(wa pili kushoto) Waziri wa Afya Mahmoud Thabiti
Kombo.

Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
(katikati) akimsikiliza Mwanamama Siti Akida Makame mkaazi wa Ziwa
Maboga aliyeruhusiwa kurudi nyumbani katika kituo cha Maradhi ya
Kipindupindu hapo Chumbuni Karakana Wilaya ya Magharibi Unguja,baada ya
kuugua maradhi hayo wakati Rais alipotembelea Kituo hicho leo asubuhi.

Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
(kulia) akisalimiana na Mkuu wa Shirika la Kimataifa la LIONS CLUBS
Kanda ya Tanzania na Uganda Bw.Hyderall Gangji wakati alipotembelea
Kituo cha Maradhi ya Kipindupindu hapo Chumbuni karakana Wilaya ya
Magharibi Unguja leo asubuhi,wengine (kushoto) Mustafa kudrati LIONS
CLUBS Tanzania na Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo.

Baadahi
ya watoa huduma na wananchi wakisubiri huduma katika Kituo cha Maradhi
ya Kipindupindu kama wanavyoonekwanwa wakati Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipotembelea
kituoni hapo Chumbuni karakana Wilaya ya Magharibi Unguja leo
asubuhi.Picha na Ikulu.
No comments:
Post a Comment