Jaji
Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman (kulia) akiwa ameongozana
na Jaji wa Mahakama Kuu ya Watu wa Jamhuri ya China, Mhe. Zhang Jiannan
(kushoto) mara baada ya kumpokea katika viwanja vya Mahakama ya Rufaa
leo jijini Dar es salaam. Mhe. Zhang Jiannan pamoja na ujumbe wake yupo
nchini kwa ziara ya kikazi kwenye Mahakama ya Tanzania kwa lengo la
kubadilishana uzoefu wa utendaji kazi na kuimarisha ushirikiano baina ya
Mahakama ya Tanzania na China.
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman (kulia) akisalimiana
na baadhi ya Majaji wa Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Watu wa China mara
baada ya kuwakaribisha Mahakama ya Rufaa leo jijini Dar es salaam.
Jaji
Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman (katikati) akizungumza
wakati wa mkutano wa pamoja kati ya Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania
na Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Watu wa China uliolenga kukuza ushirikiano
na kubadilishana uzoefu wa utendaji wa Mahakama za Tanzania na China
leo jijini Dar es salaam.
Baadhi ya Majaji wa Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Watu wa China wakifuatilia masuala mbalimbali wakati wa mkutano wa pamoja ulioongozwa na Jaji Mkuu wa Tanzania na Jaji wa Mahakama Kuu ya Watu wa Jamhuri ya China.
Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania na wale wa Mahakam Kuu ya Jamhuri ya Watu wa China wakibadilisha
uzoefu wa shughuli za kimahakama na masuala mbalimbali ya utendaji
wakati wa mkutano wa pamoja ulioongozwa na Jaji Mkuu wa Tanzania na Jaji
wa Mahakama Kuu ya Watu wa Jamhuri ya China jijini Dar es salaam.
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman (kulia) akisisitiza jambo wakati wa mkutano huo. Kushoto ni Jaji wa Mahakama Kuu ya Watu wa Jamhuri ya China, Mhe. Zhang Jiannan.
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman (kulia) akimweleza jambo Jaji wa Mahakama Kuu ya Watu wa Jamhuri ya China, Mhe. Zhang Jiannan wakati wa mkutano huo.
Jaji
wa Mahakama Kuu ya Watu wa Jamhuri ya China, Mhe. Zhang (kushoto)
akieleza namna Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Watu wa China inavyofanya kazi
leo jijini Dar es salaam wakati wa kikao cha pamoja kilichowahusisha
Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania na China. Wengine ni Jaji Mkuu wa
Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman (katikati) na Jaji Kiongozi Mhe. Shaban Lila.
Jaji
wa Mahakama Kuu ya Watu wa Jamhuri ya China, Mhe. Zhang (kushoto)
akipokea zawadi ya kinyago kutoka kwa Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe.
Mohammed Chande Othman.
Jaji
wa Mahakama Kuu ya Watu wa Jamhuri ya China, Mhe. Zhang (kushoto) akiwa
katika picha ya pamoja na Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohammed Chande
Othman mbele ya Jengo la Mahakama ya Rufaa.
Jaji
Kiongozi wa Mahakama ya Tanzania Mhe. Shaban Lila(kulia) akimweleza
jambo jaji wa Mahakamu Kuu ya Jamhuri ya Watu wa China mara baada ya
kumkaribisha Ofisini kwake Mahakama Kuu leo jijini Dar es salaam.
Jaji
Kiongozi wa Mahakama ya Tanzania Mhe. Shaban Lila(kulia) akiwa katika
mazungumzo na Jaji wa Mahakama Kuu ya China na baadhi ya Majaji kutoka
Mahakama hiyo waliomtembelea Ofisini kwake Mahakama Kuu jijini Dar es
salaam.
Jaji wa Mahakama
Kuu ya Watu wa Jamhuri ya China, Mhe. Zhang (wa pili kutoka kushoto
mbele) akiwa katika picha ya pamoja na Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe.
Mohammed Chande Othman (katikati) na baadhi ya watendaji wa Mahakama ya
Tanzania mbele ya Jengo la Mahakama ya Rufaa leo jijini Dar es salaam.
No comments:
Post a Comment