Mshindi wa
shindano la uvumbuzi wa Teknolojia mpya itakayo saidia jamii
kupatikana leo na kuzawadiwa shilingi milioni tano (5,000,000) katika
mkutano wa wadau wa teknologia unaofanyika katika ukumbi wa mkutano wa
Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Mkutano huo umeandaliwa na Bites&Bytes ukishirikiana na IBM,
TWAWEZA, FSDT pamoja na CBA, mktano huo ambao utahamasisha uendelezaji
wa mawazo mapya na uvumbuzi kwa waanzishaji wapya wa biashara na kuwapa
mwanya wa kubadilisha mawazo na wadau wengine.
Mwanzilishi
wa Bits&Bites, Lilian Madeje akiwakalibisha wageni na kufungua
mkutano wa Uvumbuzi wa Teknologia uliofanyika leo jijini Dar es Salaam
katika ukumbi wa mwalimu Nyerere.
Mwakilishi wa IBM na mstakabali wa Innovation, Ben Mann akifafanua jinsi IBM ilivyofanya kazi kwenye Teknologia hapa nchini.
Mwakilishi mwenza wa Bits&Bytes,Zuweina Farah akizungumza na wadau wa Teknologia waliokusanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi
mtendaji wa kampuni ya DTREE, Lucy Silas akizungumza na wadau wa
teknolojia na uvumbuzi wa teknologia katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere
jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya wadau wa Teknologia wakimsikiliza mtoa mada (Hayupo) pichani
jijini Dar es Salaam leo katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere.
Mwakilishi
mwenza wa Bits&Bytes,Zuweina Farah akizungumza na waandishi wa
habari kuhusiana na Teknologia na uvumbuzi wa teknologia mpya itakayo
wasaidia wanachini kufanya kazi kwa urahisi zaidi, leo katika ukumbi wa
mikutano wa mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam leo.
Amesema
kuwa leo washiriki 16 walioshiriki kuvumbua teknoloia mpya wameshiriki
katika mkutano huo na ndipo mshindi atakaye fanikiwa kushinda katika
shindano hilo atazawadiwa shilingi Milioni 5 kwa kuwa na wazo zuri
kuliko wengine ili aweze kuwa na mtaji kwaajili ya kuendeleza uvumbuzi
wake.
Mwanafunzi
mshiriki wa uvumbuzi wa Teknologia mpya itakayo wasaidia jamii, Gibson
Kawago wa shule ya Sekondari ya huko Arusha akiwa amegundua taa za miale
ya jua(Solar Power) zinazoweza kuchaji simu za Smati kwa zaidi ya masaa
nane.
Mwakilishi
wa Fist Financial Sector Deeping(FSDT), Revis Mushi akizungumza na
waaandishi wa habari katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es
Salaam leo. Amesema kuwa mkutano huo utasaidia jamii na wananchi kwa
ujumla kusaidia kupata mfumo mwepesi wa Teknologia.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Atamizi (DTB) ambayo ipo tume ya Sayansi, George Mulamula
akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo katika
ukumbi wa Mwalimu Nyerere kuhusiana na amesema kuwa Tume ya Sayansi
imeungana katika mkutano wa Teknologia ili kuwapa ujuzi zaidi Vijana.
Pia amesema kuwa katika Tume ya Sayansi wameweza kuvumbua mfumo wa Max
Malipo na wa mfumo wa kudahili wanafunzi wa TCU.
Mshiriki na Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Jangwani, Necta Richard akizungumza na waandishi wa habari leo mara baada ya mkutano wa Teknologia uliofanyika jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya washiriki katika mkutano wa Teknologia.
Washiriki.
No comments:
Post a Comment