Kikosi cha Yanga.
Kikosi cha Azam.
Mshambuliaji
wa Timu ya Azam, Kipre Tchetche akiwatoka Mabeki wa Timu ya Yanga,
Mbuyu Twite na Vicent Bossou, wakati wa Mtanange wa Ligi Kuu ya Vodacom
Tanzania Bara, uliopigwa Jioni ya leo kwenye Uwanja wa Taifa, Jijini Dar
es Salaam. Hadi kipenga cha mwisho kikilizwa na Mwamuzi, Kennedy
Mapunda, timu zote zilikuwa zimefungana Bao 2-2 na kuzifanya timu hizo
zikiondoka uwanjani hapo zikiwa na Pointi sawa ila Yanga ikiongoza Ligi
kwa uwingi wa Magoli ya kufunga.
Beki wa Yanga, Juma Abdul akiondosha hatari iliyokuwa ikielekezwa langoni kwao na Mchezaji wa Azam, Farid Mussa.
Mshambuliaji wa Azam, John Bocco akiangalia namna ya kumtoka Beki wa Yanga.
Mshambuliaji
wa Yanga, Donald Ngoma akionyesha umahiri wake wa kumtoka beki wa Azam,
Said Morad huku akiwa kadhibitiwa kweli kweli.
Chukua huyooo....
Mchezaji
wa Azam, Shomari Kapombe akiruka daruga la Beki wa Yanga, Vicent
Bossou, wakati wa Mtanange wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara,
uliopigwa Jioni ya leo kwenye Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es Salaam.
Hadi mwisho wa mchezi, Azam 2 - 2 Yanga.
No comments:
Post a Comment