Matukio : Sherehe ya Kuapishwa Rais wa Zanzibar Dk. Shein - Wazalendo 25 Blog

Breaking

Glory to Story.


Post Top Ad


25 Mar 2016

Matukio : Sherehe ya Kuapishwa Rais wa Zanzibar Dk. Shein

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akitia saini hati ya kiapo mbele ya Jaji Mkuu Mhe,Omar Othman Makungu baadanya kumalizikika kwa zoezi hilo lililofanyika leo katika Uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja(katikati) Katibu Mkuu Kiongozi Dkt.Abdulhamid Yahya Mzee. 
WanaChama cha Mapinduzi na Wananchi wakiwa pamoja wakisherehekea kuapishwa kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein leo katika uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja,pia wakiwepo Waandishi wa Habari kushuhudia mambo mbali mbali yanayoendelea katika zoezi la kuapishwa kwa Rais.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifuatana na Makamanda wakati alipokuwa akikagua gwaride la Vikosi vya Brass Band leo katika uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja,baada ya kuapishwa rasmi kwa kuongoza Zanzibar katika kipindi cha Pili cha Awamu ya saba.
Viongozi mbali mbali wakisimama wakati wimbo wa Taifa ukipigwa katika sherehe za Kuapishwa kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.ALi Mohamed Shein Uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja.
 
Waaandishi wa Habari Wapigapicha wakijaribu kufanikisha kazi yao kupata matukio mbali mbali wakati wa Sherehe za kumuapisha kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.ALi Mohamed Shein katika Uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akikagua gwaride la Vikosi vya Ulinzi na Usalama lenye muundo wa ALfa katika Uwanja wa Amaan Studium baada ya kuapishwa.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiwapungia mkono wananchi baada ya zoezi la kuapishwa pamoja na kukagua gwaride la Vikosi vya Ulinzi na Usalama lenye muundo wa ALfa unaoashiria mwanzo wa Uongozi wake kwa kipindi cha pili katika Uwanja wa Amaan Studium baada ya kuapishwa rasmi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akipeana mkono na Kamishna wa Polisi Zanzibar Hamdani Omar Makame wakati aliposalimiana na Wakuu wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama baada ya kumalizika zoezi la kuapishwa katika Uwanja wa Amaan Studium.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akipeana mkono na Mkuu wa KMKM Hassan MUssa Komodoo wakati aliposalimiana na Wakuu wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama baada ya kumalizika zoezi la kuapishwa katika Uwanja wa Amaan Studium.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akipeana mkono na Kaimu Mkuu wa JKU Kanali Ali Mtumweni Hamadi wakati aliposalimiana na Wakuu wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama baada ya kumalizika zoezi la kuapishwa katika Uwanja wa Amaan Studium.[Picha na Ikulu.]

Post Top Ad