Kaimu
Kamishna wa TRA Alphayo Kidata akizungumza na waandishi wa
habari(Hawapo pichani) katika mkutano wa kuota taarifa juu ya ukusanyaji
wa kodi kwa mwezi Februari.
Kaimu
Kamishna wa TRA Alphayo Kidata akifafanua jambo waandishi wa
habari(Hawapo pichani) kuhusu mpango wa Serikali kuwasaidia wananchi wa
kipato cha chini ili waweze kumudu kulipa kodi ,kulia ni Kaimu Kamishna
wa kodi za Ndani wa Mamlaka hiyo Salum Yusufu.
…………………………………….
Na Raymond Mushumbusi, MAELEZO
Serikali
ipo kwenye mpango wa kuunda Mamlaka ya Mapato Kuu ya Taifa nje ya
Mamlaka ya Mapato ya Tanzania (TRA) iliyopo kwa sasa ili kuondokana na
malalamiko ya kero za kodi kwa wananchi wenye kipato cha chini.
Hayo
yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Kaimu Kamishna wa Mamlaka ya
Mapato Tanzania Alphayo Kidata alipokuwa akifafanua kuhusu juhudi za
Serikali katika kuwasaidia wananchi wa kipato cha chini kuweza kumudu
kulipa kiwango cha kodi kinachowekwa na na Mamlaka hiyo.
“
Napenda kuwambia umma wa watanzania kwamba Serikali ya Awamu ya tano
inawajali watu wake na ndio maana imeona kuwa kuna haja ya kuunda
Mamlaka moja ya utozaji wa kodi itakayojumuisha taasisi zote
zinazohusika na kukusanya mapato nje ya kodi na ushuru ili kuondokana na
malalamiko mengi ya wananchi juu ya utozaji wa kodi hasa katika
Halmashauri zetu”Alisema Kidata.
Kamishna
Kidata amesema kuwa katika dunia hii hakuna Serikali ambayo
imechaguliwa na wananchi ikaamua tu kuwakandamiza wananchi wake katika
jambo lolote lile hivyo basi kwa sasaserikali ipo katika mchakato wa
kuunda Mamlaka hiyo ambayo itasaidia kuweka viwango vya kodi ambavyo
wananchi wa hali ya chini watamudu kulipa kutokana na biashara au kazi
wanazozifanya.
Kamishna
huyo ameongeza kuwa Mamlaka yake kwa kushirikiana na mamlaka nyingine
zinazokusanya kodi katika Halmashauri nchini watahakikisha wanalipatia
ufumbuzi suala la kero ya kodi kwa wananchi wa hali ya chini kwa kupata
muafaka ambao utasaidia pande zote mbili bila kukandamiza upande wowote
iwe Serikali ama mwananchi wa kawaida.
Mamlaka
ya Mapato Tanzania (TRA) imekuwa na rekodi nzuri ya ukusanyaji wa kodi
ila kumekuwa na malalamiko mengi kutoka kwa wananchi kuhusu kodi ambazo
zimekuwa kero na hazina tija. Hivyo Serikali imejipanga kuiongezea nguvu
Mamlaka hiyo kwa kuipa uwezo wa kukusanya na mapato ambayo hayatokani
na kodi toka katika wizara, mashirika,tasisi za serikalina Halmashauri
zote nchini.
No comments:
Post a Comment