Msafara wa Rais wa Vietnam ukiwasili katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam 9 Machi, 2016.
|
Rais
wa Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang (kulia) akiwasili katika viwanja vya
Ikulu Jijini Dar es Salaam 9 Machi, 2016 kwa ajili ya ziara yake ya
kikazi yenye kuendeleza mahusiano baina ya Tanzania na Vietnam.
|
Mke wa Rais wa Vietnam, Bi. Mai Thi Hanh (mwenye gauni jekundu) akipokea ua toka kwa mtoto mara alipowasili katika
viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam 9 Machi, 2016 akiwa ameambatana
na mmewe kwa ajili ya ziara yake ya kikazi yenye kuendeleza mahusiano
baina ya Tanzania na Vietnam.
|
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Joseph Magufuli (wa
pili kulia) akimkaribisha mgeni wake Rais wa Vietnam, Mhe. Truong Tan
Sang mara alipowasili katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam 9 Machi, 2016
|
Rais
wa Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang (wa pili kulia) akisalimiana na Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan
(mwenye koti la drafti) mara alipowasili katika
viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam 9 Machi, 2016. Wa kwanza kulia
ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Joseph
Magufuli.
|
Rais
wa Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang (wa tatu kulia) akisalimiana na Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa
(wa tatu kushoto) mara alipowasili katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam 9 Machi, 2016.
|
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Joseph Magufuli (wa pili kulia) pamoja na Rais
wa Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang wakipanda jukwaani kwa ajili ya
kuimbiwa nyimbo za taifa kabla ya kukagua gwaride 9 Machi, 2016 Jijini
Dar es Salaam.
|
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Joseph Magufuli (kulia) pamoja na Rais
wa Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang wakiwa jukwaani kwa ajili ya kuimbiwa
nyimbo za taifa kabla ya kukagua gwaride 9 Machi, 2016 Jijini Dar es
Salaam.
|
Rais
wa Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang(mwenye tai nyekundu) akikagua gwaride
mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam 9
Machi, 2016.
|
Umati
wa watu wakiwa ndani Ikulu Jijini Dr es Salaam 9 Machi, 2016 kwa ajili
ya kumpokea Rais wa Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang aliyewasili jana kwa
ajili ya ziara yake ya kazi nchini Tanzania.
|
Rais wa Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang (kushoto) pamoja na mkewe mama
Mai
Thi Hanh (mwenye gauni jekundu) wakiingia ndani ya Ikulu Jijini Dar es
Salaam 9 Machi, 2016 kwa mara ya kwanza kwa ajili ya ziara ya kikazi
yenye kukuza uhusiano baina ya Tanzania na Vietnam
|
Mke
wa Rais wa Vietnam, Bi. Mai Thi Hanh (mwenye gauni jekundu)
akisalimiana na akina mama waliompokea mara alipotembelea katika ofisi
za mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Janeth Magufuli 9
Machi, Ikulu Jijini Dar es Salaam.
|
Mke wa Rais wa Vietnam, Bi. Mai Thi Hanh akisaini kitabu cha wageni mara alipowasili katika ofisi za mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Janeth Magufuli (kulia) 9 Machi, Ikulu Jijini Dar es Salaam.
|
Mke wa Rais wa Vietnam, Bi. Mai Thi Hanh pamoja na Mama Janeth Magufuli wakifurahia jambo 9 Machi, Ikulu Jijini Dar es Salaam.
|
Mke
wa Rais wa Vietnam, Bi. Mai Thi Hanh (kushoto) akifurahia zawadi ya
kinyago cha kuchonga alichokabidhiwa na mwenyeji wake mama Janeth
Magufuli kama zawadi 9 Machi, 2016 katika ofisi za Mke wa Rais Jijini
Dar es Salaam.
|
Mke
wa Rais wa Vietnam, Bi. Mai Thi Hanh (kushoto) akimpa zawadi mama
Janeth Magufuli ikiwa shukurani yake mara alipotembelea katika ofisi
yake 9 Machi, 2016 Jijini Dar es Salaam.
|
Mama Janeth Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na mgeni wake mama Mai Thi Hanh mara baada ya kutembelea katika ofisi hiyo leo 9 Machi, 2016 Ikulu Jijini Dar es Salaam.
|
Mke
wa Rais wa Vietnam, Bi. Mai Thi Hanh (mwenye gauni jekundu) akipata
maelezo kuhusu nyaraka mbalimbali ziliko katika Makumbusho ya Taifa
Jijini Dar es Salaam leo 9 Machi, 2016.(Picha zote na Benedict Liwenga-Maelezo)
|
No comments:
Post a Comment